Majina ya Nyongeza ya Walioitwa Kwenye Usaili Benki Kuu ya Tanzania

Majina ya Nyongeza ya Walioitwa Kwenye Usaili Benki Kuu ya Tanzania
Majina ya Nyongeza ya Walioitwa Kwenye Usaili Benki Kuu ya Tanzania 14-02-2025
Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anapenda kuwataarifu waombaji
kazi wote walioomba kazi kuwa usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) unatarajiwa kuendeshwa kuanzia
tarehe 15-02-2025 hadi 24-03-2025.
Wasailiwa watakaofuzu usaili huu na kwenda katika hatua zinazofuata
watatakiwa kushiriki katika usaili wa vitendo au/na mahojiano kwa tarehe iliyoanishwa au kama watakavyotaarifiwa kwa wakati husika.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wa kuandika/mchujo (Aptitude Test) wanapaswa kuzingatia maelekezo
yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji/shehia anakotoka msailiwa.
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI,
Astashahada, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na vyeti vingine (kutegemeana na nafasi aliyoomba). - Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za
matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA
HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. - Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na
Mamlaka husika (kama TCU, NACTVET au NECTA) - Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Wasailiwa wa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja
na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi. - Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
MUHIMU: Wasailiwa watakao shindwa kuwasilisha nyaraka zilizokamilika kama zilivyoainishwa katika
kipengele na. 2, 3, 4, 8 na 10 hawataruhusiwa kuendelea na usaili.
KUITWA KWENYE USAILI BENKI KUU YA TANZANIA MAJINA YA NYONGEZA 14-02-2025
Majina 4089 ya Walioitwa Kwenye Usaili BOT, Kuitwa Kwenye Usaili Benki Kuu ya Tanzania
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Majina ya Nyongeza ya Walioitwa Kwenye Usaili Benki Kuu ya Tanzania