MAJINA ya Wagombea Uchaguzi Mkuu CWT 2025/2030

MAJINA ya Wagombea Uchaguzi Mkuu CWT 2025/2030
MAJINA ya Wagombea Uchaguzi Mkuu CWT 2025/2030
Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) inapenda kuwataarifu walimu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa chama kinatarajia kufanya Mkutano Mkuu wa saba utakaofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia 28 na 29 May Jijini Dodoma.
Pamoja na mambo mengine Mkutano Mkuu huo utafanya uchaguzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali kwa Ngazi ya Taifa
Hii ni baada ya kukamilika kwa chaguzi zilizokuwa zikiendelea nchini kote kwa ngazi za shule (Tawi), Wilaya na Mikoa na sasa chama kitakamilisha Ngazi ya Taifa.
Miongoni mwa nafasi za kitaifa zinazotarajiwa kufanyiwa uchaguzi ni pamoja na:-
- Rais wa CWT
- Makamu wa rais CWT
- Katibu Mkuu wa CWT
- Naibu katibu mkuu CWT
- Mweka hazina CWT
- Mwakilishi wa walimu wenye ulemavu
- Mwakilishi wa walimu vijana
- Mwakilishi wa Walimu wanawake
- Mjumbe wa kamati ya utendaji TUCTA kutoka CWT
- Wadhamini watatu
- Vitengo mbalimbali vya chama
Chama kinawakaribisha wajumbe wa Mkutano Mkuu Kushiriki tukio lao hilo muhimu na la kihistoria.
Aidha orodha ya wagombea wa nafasi imeambatanishwa hapa chini.

Tags: MAJINA ya Wagombea Uchaguzi Mkuu Chama Cha Walimu Tanzania 2025/2030, MAJINA ya Wagombea Uchaguzi Mkuu CWT 2025/2030
