MAJINA ya Walioitwa Kazini Jeshi la Polisi Tanzania 2025

MAJINA ya Walioitwa Kazini Jeshi la Polisi Tanzania 2025
MAJINA ya Walioitwa Kazini Jeshi la Polisi Tanzania 2025, Tangazo la kuripoti shule ya polisi moshi kwa vijana waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania 2025.
Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 12/06/2025 hadi tarehe 14/06/2025 kwaajili ya kuhudhuria mafunzo.
Vijana waliofanyiwa usaili Dar es Salaam kwenye Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wataripoti jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa Road tarehe 12/06/2025 saa 12.00 asubuhi kwaajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwaajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
Vilevile, vijana waliofanyia usaili Zanzibar (Unguja na Pemba) wanatakiwa waripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 11/06/2025 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari.
Aidha, vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:
- Traki suti (track suit) rangi ya bluu (blue) yenye ufito mweupe, fulana
(t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi, l raba, soksi nyeusi, bukta mbili (2) za bluu (blue) kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja nansanduku la chuma (Tranka) la rangi ya bluu. - Chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za rangi ya bluu mpauko (light blue) jozi mbili (Shuka 4), pasi ya mkaa na blanket moja la kijivu lisilo na maua na sio duveti.
- Kikombe cha plastiki ambacho kimetengenezwa kwa matirio ya mfupa (Cream light), Sahani moja aina ya ‘steel dish plate’.
- Vifaa vya usafi: Sururu moja lenye mpini, ndoo mbili ndogo na fagio la chelewa.
- Kadi ya bima ya Afya (NHIF) kama anayo au fedha taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi za bima ya Afya.
- Vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates), cheti halisi cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA), Nakala za kadi za NIDA au namba za Utambulisho wa Taifa (NIDA) za wazazi na watu wa karibu upande wa Baba na Mama (kama vile Baba, Baba mkubwa, Baba mdogo, Shangazi, Mama, Mama mkubwa, Mama mdogo, Mjomba, Babu nk), passport size 6 (background blue), na nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa hapo juu.
- Fedha za kujikimu.
- Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi ukiwa na simu ya mkononi. Yeyote atakayepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano.
- Kwa yeyote atakayeripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 14/06/2025 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo.
Orodha ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa hapa chini kwenye PDF.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: MAJINA ya Walioitwa Kazini Jeshi la Polisi Tanzania 2025