Majina ya walioitwa Kazini, Wizara ya Afya, waliopata Ajira Wizara ya Afya

Majina ya walioitwa Kazini, Wizara ya Afya, waliopata Ajira Wizara ya Afya
Majina ya walioitwa Kazini, Wizara ya Afya, waliopata Ajira Wizara ya Afya
Katibu Mkuu Wizara ya Afya anapenda kuwataarifu waombaji wote waliofaulu usaili wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na kupangiwa kuripoti Wizara ya Afya kwamba, waripoti katika Ukumbi wa Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi, Mirembe
DODOMA ( DIHAS) ili kukamilisha taratibu za ajira kama tarehe zinavyoonesha kwenye tangazo.
Waajiriwa wote wanatakiwa kufika na vyeti halisi (Original) nakala 2 kwa kila cheti ambacho kilitumika wakati wa kuomba ajira ikiwa ni pamoja na:
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Wasifu binafsi (CV).
- Picha mbili (2) Passport size.
- Nakala ya Kitambulisho/namba ya uraia (NIDA)
- Nakala ya vyeti vya elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne na Sita).
- Nakala ya vyeti vya taaluma pamoja na Transcript.
- Nakala ya Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo. (Internship).
- Nakala ya cheti cha usajili kutoka Baraza na Bodi husika (Valid Licence).
- Nakala ya Ithibati ya vyeti vya elimu na taaluma (Accreditation and Equivalence) kutoka TCU na NECTA kwa waliosoma vyuo vya nje ya nchi pamoja na wale
waliosoma Sekondari nje ya nchi/Mitaala ya nje. - Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa hakikisha unawasilisha Kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na kusajiliwa na Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makazi. - Kuripoti vituo vya kazi watakavyopangiwa katika muda wa siku 14 baada ya kupokea barua ya ajira.
Waajiriwa watakaoshindwa kuripotikatika vituo walivyopangiwa kwa muda uliopangwa, nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine wa kada husika.
Aidha, yeyote atakayeripoti na Transcript tu au kuwa na nakala pungufu za vielelezo tajwa hapo juu hatapokelewa.
Orodha ya majina ya waajiriwa walioitwa kuripoti Kazini imeambatanishwa kwenye PDF hapa chini;
ORODHA YA WAAJIRIWA WAPYA NA TAREHE WANAZOTAKIWA KURIPOTI WIZARA YA AFYA DOWNLOAD PDF DOCUMENT HAPA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Majina ya walioitwa Kazini, waliopata Ajira Wizara ya Afya, Wizara ya Afya