MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Tanganyika District Council 29/05/2025

MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Tanganyika District Council 29/05/2025
MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Tanganyika District Council 29/05/2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Tanganyika anapenda kuwatangazia wafuatao kufika kwenye usaili kwaajili ya nafasi ya Fundi Sanifu Ujenzi II nafasi 1, Fundi Sanifu Magari II nafasi 1, Afisa Habari Msaidizi II nafasi 1 na Makarani wa Mapato nafasi 50 aliyotangaza kupitia tangazo lenye Kumb. Na. KTV/MDC/A.40/3/30 la tarehe 02.03.2025.
Usaili huo utafanyika tarehe 04 hadi 05.06.2025 katika Bwalo la Shule ya Sekondari ya Kabungu.
MASHARTI KWA UJUMLA:
- Wahusika wanatakiwa kufika na vyeti halisi vya shule, chuo na kuzaliwa.
- Usaili utaanza saa mbili kamili (2.00) asubuhi. Ukumbi upo katika sekondari iliyotajwa hapo juu, Shule iko karibu na Geti la Mapato Kabungu katika barabara inayokwenda Kigoma takribani kilometa kumi (10) kutoka Mpanda Mjini.
- Waombaji watajigharamia wenyewe usafiri, malazi na chakula.
- Waombaji wanatakiwa kufika na mojawapo ya nyaraka/vitambulisho vifuatavyo.
- Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
- Leseni ya udereva ambayo haijakwisha muda wa matumizi.
- Kadi ya Mpiga kura.
- HAti ya kusafiria (Passport).
- Kitambulisho ya makazi.
- Barua ya Mtendaji wa Kata/Kijiji/Mtaa yenye picha na mhuri wa Mtendaji husika.
Usaili wa kuandika (mchujo) kwa kada zote utafanyika tarehe 04.06.2025 na usaili wa ana kwa ana (Mahojiano) utafanyika tarehe 05.06.2025 kwa watakaofaulu usaili wa kuandika (mchujo).
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: MAJINA ya Walioitwa Kwenye Usaili Tanganyika District Council 29/05/2025
