MAMBO Muhimu ya Kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili Ajira Portal

MAMBO Muhimu ya Kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili Ajira Portal
MAMBO Muhimu ya Kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili Ajira Portal
Kupitia Makala hii utaweza kujifunza Mambo Muhimu ambayo unapaswa kuyazingatia unapoitwa kwenye Usaili Ajira Portal (PSRS).
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ndicho chombo pekee kwa mujibu wa sheria chenye Mamlaka ya kuajiri watu katika Utumishi wa Umma kwa kuzingatia SERA, SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU zinazohusu Ajira katika Utumishi wa Umma.
Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa
Umma unazingatia sifa, taaluma, ushindani, uwazi, na usawa kwa mujibu wa SERA, SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU zinazohusu Ajira katika Utumishi wa Umma.
Aidha Sekretarieti ya Ajira huendesha saili mbalimbali ili kupata wataalamu wenye tija kulingana na nafasi za ajira zilizotangazwa.
Saili za vitendo hufanyika kwa kada zenye mahitaji ya kubaini uwezo wa kutumia nyenzo mahsusi, ili kupima uwezo wa ujuzi wa utendaji kazi.
Hivo ni muhimu kupakia taarifa binafsi na za kitaaluma kwenye mfumo wa AJIRA PORTAL ili kuweza kuomba kazi pindi zitakapotangazwa.
Hizi hapa ni nyaraka Muhimu wakati wa kwenda kwenye Usaili Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS).
Nyaraka hizo ni kama zilivyoainishwa hapa chini;
- Cheti halisi cha kuzaliwa
- Kitambulisho cha Taifa, Kitambulisho Cha Mkazi, Hati ya kusafiria, Kadi ya Mpiga Kura, Leseni ya Udereva au Barua kutoka Serikali ya Mtaa
- Vyeti halisi vya kitaaluma
- Hati ya kiapo, endapo majina yanatofautiana kwenye nyaraka.
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakishe vyeti vya vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika kama (TCU, NACTE na NECTA.
Gusa HAPA Kupata Ajira zote zinazotangazwa Kila Siku
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Mambo Muhimu unapoitwa kwenye Usaili UTUMISHI, MAMBO Muhimu ya Kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili Ajira Portal, Mambo Muhimu ya Kuzingatia unapoitwa kwenye Usaili UTUMISHI