MAMBO Muhimu ya Kuzingatia Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025

MAMBO Muhimu ya Kuzingatia Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025
MAMBO Muhimu ya Kuzingatia Walioitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025
Mkuu wa Jeshi la Polisi ametangaza tarehe za Usaili kwa vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi kuwa utafanyika kuanzia tarehe 28/4/2025 saa 07:00 asubuhi hadi tarehe 11/5/2025 kote nchini.
Kuelekea usaili huo, Kuna mambo muhimu ambayo wewe msailiwa unapaswa Kuyazingatia ili kukidhi matakwa ya Usaili wa Jeshi hilo.
Mambo muhimu ya Kuzingatia ambayo yametajwa na Mkuu huyo wa Jeshi ni kama ifuatavyo;
Kwa wasailiwa wenye Elimu ya Shahada, Stashahada na Astashahada.
- Hawa usaili wao utafanyika jijini Dar es Salaam katika uwanja wa gwaride uliopo Kambi ya Polisi (Police Barracks) barabara ya Kilwa nyuma ya kituo cha Polisi Kilwa
Road.
Kwa Upande wa wasailiwa wenye Elimu ya kidato cha Nne na cha Sita.
- Usaili wao utafanyika kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliyoichagua wakati wa kutuma maombi ya Ajira.
Kwa wasailiwa wa Zanzibar wenye Elimu ya Shahada, Stashahada,
Astashahada, Kidato Cha Sita na Nne.
- Usaili wao utafanyika Zanzibar ambapo kwa walioko mikoa ya Unguja, usaili utafanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) na Mikoa ya Pemba usaili wao utafanyika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba (Chakechake).
Vitu vya kwenda navyo kwenye Usaili wa Jeshi la Polisi 2025
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi amesema kuwa kila msailiwa atalazimika kufika eneo lake la usaili akiwa na vyeti halisi vya taaluma (Academic certificates), Cheti Cha Kuzaliwa, Kitambulisho Cha Taifa cha NIDA au namba ya NIDA pamoja na nguo na viatu vya michezo.
Aidha Wasailiwa watakaofika kwenye usaili baada ya tarehe 28/04/2025 hawapokelewa.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: MAMBO Muhimu ya Kuzingatia Waliolitwa Kwenye Usaili Jeshi la Polisi 2025