Maslahi ya Walimu Kupitiwa upya Rais Samia

Filed in Elimu by on February 2, 2025 0 Comments
     
Maslahi ya Walimu Kupitiwa upya Rais Samia

Maslahi ya Walimu Kupitiwa upya Rais Samia

Maslahi ya Walimu Kupitiwa upya Rais Samia

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itapitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hiyo kama Mama wa taaluma zote Duniani.

Akiongea February 01,2025 wakati akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2024 Jijini Dodoma, Rais Samia amesema kuwa “Tutapitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahiki kada hii kama Mama wa taaluma zote Duniani”

“Sera hii inamaanisha upanuzi wa miundombinu ya elimu nchini, hivyo niitake TAMISEMI iandae mkakati wa kutekeleza sera hii kwa ujenzi wa miundombinu nchini, mafanikio ya sera hii yatategemea sana utekelezaji hivyo kila mmoja atekeleze wajibu wake, Watoto wahudhurie masomo, Wazazi wahakikishe Watoto wanafuatilia masomo na Serikali tusimamie ubora wa elimu na kuinua hadhi ya Mwalimu nchini “

“Utekelezaji wa sera hii unahitaji fedha nyingi na Mimi nilijipiga kifua nikasema Waziri fanyeni Mungu anajua atatufungulia wapi tutapata tutaendelea lakini pa kwanza pa kufunua ni ndani lazima tuongeze ukusanyaji wa mapato ndani ya nchi, kwa hiyo nisisitize msemo wetu maarufu ukinunua omba risiti na ukiuza toa risiti na tusimamie kwa pamoja wanaokwepa kulipa kodi”

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!