MASWALI ya Usaili Ajira za INEC, Maswali ya usaili BVR

Filed in Usaili by on February 25, 2025 0 Comments
     
MASWALI ya Usaili Ajira za INEC, Maswali ya usaili BVR

MASWALI ya Usaili Ajira za INEC, Maswali ya usaili BVR

MASWALI ya Usaili Ajira za INEC, Maswali ya usaili BVR

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 74(7) na (11) ya Katiba na kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, Tume ni idara huru inayojitegemea na inafanya maamuzi yake rasmi kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa vikao.

Katika kutekeleza majukumu yake ya kikatiba, Tume haitalazimika kufuata amri au maagizo ya mtu yeyote au idara yoyote ya Serikali au maoni ya chama chochote cha siasa.

Kupitia Makala hii tumekuandalia orodha ya maswali ambayo yanaulizwa mara Kwa mara pale wasailiwa wanapoitwa kwenye Usaili Kutoka Halmashauri Mbalimbali nchini.

1:Nini kitatokea ikiwa mtu amejiandikisha zaidi ya mara moja?

Jibu: Ni kosa la jinai mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja, na ikitokea, mtu ataadhibiwa kulingana na sheria za Uchaguzi.

2:Je Mawakala wa vyama vya Siasa wanaruhusiwa kuangalia zoezi la uandikishaji wapiga kura kituoni?

Jibu: Ndio, Mawakala wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wanaruhusiwa kuwa na mwangalizi mmoja kwa kila kituo cha Uandikishaji Wapiga kura.

3:Kwa nini Ujiandikishe kuwa Mpiga Kura?

Jibu: Ili kuweza kutimiza haki yako katika Kupiga Kura siku ya Kura ya Maoni na Uchaguzi, Kuweza kushiriki katika uongozi Nchi yako.

4:Nani anapoteza sifa za kuandikishwa kuwa Mpiga kura?

Jibu: Ikiwa ana Uraia wa Nchi nyingine yaani sio Raia wa Tanzania, Amehukumiwa kifungo cha zaidi ya Miezi Sita, Amehukumiwa kifo na Mahakama za Tanzania,  Amethibitika kuwa hana Akili timamu.

5:Uteuzi ni nini?

Jibu: Uteuzi ni sehemu ya Mchakato wa Uchaguzi, ambapo Tume inamteua Mgombea Kugombea nafasi katika Uchaguzi. Mgombe huyo ni sharti awe ameteuliwa na chama chake cha Siasa.

Afisa Mwandikishaji maana yake ni mtu aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 7 cha Sheria na inajumuisha afisa mwandikishaji msaidizi;

Afisa wa Tume maana yake ni mwajiriwa wa Tume;

Chama cha Siasa maana yake ni chama cha siasa kilichosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama vya Siasa;

Daftari maana yake ni Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoanzishwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria;

Daftari la Awali la Wapiga Kura maana yake ni daftari
lililoanzishwa chini ya kifungu cha 11 cha Sheria;

jimbo maana yake ni jimbo la uchaguzi kwa madhumuni ya uchaguzi wa Mbunge;

Kadi ya Mpiga Kura maana yake ni kadi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria, ikithibitisha kwamba mtu aliyetajwa katika kadi hiyo ameandikishwa kuwa mpiga kura;

Kata maana yake ni mgawanyo wa mamlaka katika mamlaka za serikali za mitaa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji);

Kiapo cha kutunza siri maana yake ni kiapo kinachozuia kutoa taarifa yoyote ya mtu aliyeomba kuandikishwa au jambo lolote linalohusu uandikishaji isipokuwa kwa madhumuni yaliyoidhinishwa kwa mujibu wa sheria

kijiji itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya)

Kitongoji itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya);

Kituo Cha Uandikishaji maana yake ni kituo kilichoanzishwa na Tume kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura;

Mfungwa itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Magereza na kwa madhumuni ya Kanuni hizi, inajumuisha mahabusu Sheria Na. 2 ya Mwaka 2024

Mkurugenzi wa Uchaguzi itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi; Sura ya 288

Mtaa itakuwa na maana sawa kama ilivyotafsiriwa katika
Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji);

Mwangalizi Wa Uandikishaji maana yake ni mwangalizi wa uandikishaji wa ndani au wa kimataifa aliyeidhinishwa na Tume;

Mwandishi Msaidizi maana yake ni mtu aliyeteuliwa na afisa mwandikishaji chini ya kanuni ya 11 na itajumuisha mwendeshaji wa kifaa cha bayometriki;

Namba ya kipekee ya utambuzi wa mpiga kura maana
yake ni namba ya kudumu ya utambulisho wa mpiga kura.

Taarifa za uandikishaji maana yake ni taarifa za mpiga kura zilizoandaliwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria;

Tume maana yake ni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

Uboreshaji maana yake ni uandikishaji wa wapiga kura wapya wenye sifa, ufanyaji wa marekebisho ya taarifa za wapiga kura, uhamishaji wa taarifa za wapiga kura, utoaji wa kadi mpya kwa wapiga kura na ufutaji wa majina ya waliopoteza sifa kwenye

Daftari uchaguzi maana yake-
(a) iwapo ni kumchagua Rais, ni uchaguzi wa Rais;
(b) iwapo ni kumchagua Mbunge, ni uchaguzi wa Mbunge, na inajumuisha uchaguzi mdogo; na
(c) iwapo ni kumchagua Diwani, ni uchaguzi wa Diwani, na inajumuisha uchaguzi mdogo;

Vifaa Vya Uandikishaji maana yake ni vifaa vilivyopata kibali cha Tume kwa lengo la kutumika katika uandikishaji

Wakala Wa Uandikishaji maana yake ni mtu aliyeteuliwa na chama cha siasa kuwa wakala chini ya kifungu cha 17 cha Sheria; na

Watendaji Wa Uandikishaji  inajumuisha mratibu wa uandikishaji wa mkoa, afisa mwandikishaji, afisa mwandikishaji msaidizi, mwandishi msaidizi, mwendeshaji wa kifaa cha bayometriki na watendaji wengine watakaoteuliwa na Tume.

BVR ni nini?
Biometric Voter Registration (BVR) ni njia ya kusajili wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya kompyuta kunasa data za maumbile ya mtu kwa vile jina, umri, jinsia, alama za vidole na uso. Teknolojia hii inatumika kuthibitisha uhalisi wa wapiga kura na kuhakikisha uwazi na usadiki zaidi wa uchaguzi.

Je, vipi vifaa muhimu vya BVR?
Vifaa vya BVR ni pamoja na:
a) Kompyuta ndogo ya mkononi
b) Skena ya kuchukua alama za vidole
c) Kamera
d) Programu ya usajili
e) Hifadhi ya umeme
f) Pazia la nyuma la kuchukulia picha

Nini inaifanya BVR bora zaidi katika kuunda sajili ya kuaminika?
Habari za kibinafsi zinazonaswa na BVR ni za kipekee kwa kila mtu na haziwezi kutumiwa na mwingine. Hii inasaidia kuunda sajili ya kuaminika. BVR inahitaji kila mpiga kura kufika mwenyewe katika kituo cha kura ili kuhakikisha ni wapiga kura tu hakika ambao wamesajiliwa na wanaofika wenyewe siku ya uchaguzi ndio wanapiga kura.

Ni manufaa yapi ya BVR yaweza kulinganishwa dhidi ya sajili ya karatasi inayotumia mbinu ya Optical Mark Reader (OMR)?
BVR ina manufaa yafuatayo dhidi ya mbinu za zamani za usajili;

a) Kipekee: BVR hunasa maelezo ya kipekee ya mtu. Ni vigumu kabisa kuwa na watu wawili walio na data sawia za maumbile.

b) Haiwezi kutumiwa na watu wawili: Data za maumbile zinazonaswa na BVR ni hususan za mtu binafsi na haziwezi kunakiliwa ama kuwa za watu wawili (huwezi kumpa mtu nakala ya uso ama vidole vyako!) hii haikuwa hivyo katika sajili ya awali ambapo nambari za vitambulisho ama pasipoti zilizotumika kumtambua mpiga kura zilikuwa rahisi kubuni ama kunakili.

c) Haiwezi kunakiliwa: Ni vigumu kabisa kubuni ama kudanganya maumbile. Hii inahakikisha maelezo yanayotolewa ni ya mtu aliye hai.

d) Haiwezi kupotea: Maumbile ya mtu yaweza tu kupotea katika ajali mbaya kabisa kinyume na sajili ya karatasi ambapo mpiga kura aweza kupoteza kadi yake ama kitambulisho na kikatumiwa na mlaghai kupigia kura.

e) Sahihu: BVR hunasa maelezo ya mpiga kura moja kwa moja katika kifaa cha teknolojia. Mpiga kura huthibitisha data hii kabla haijaakibishwa. Hii huchangia kuwepo kwa sajili sahihi nay a kuaminika.

f) Haraka: Mbinu hii hutoa fursa ya kunaasa maelezo kwa haraka na data hiyo haihitaji kuchambuliwa na kutengenezwa tena. Hii inakuwa haraka kuunganisha sajili ya wapiga kura kinyume na mbinu ya zamani iliyohitaji data kukaguliwa na kutengenezwa.

g) Epesi na sawasawa: BVR inahakikisha mpiga kura anatambulika kwa wepesi na sawasawa na ni msingi wa uchaguzi wowote wa kuaminika. Mbinu hii inatoa viwango vya juu kabisa vya usalama wa kupiga kura na inazuia udanganyifu katika uchaguzi.

Je, BVR ni salama?

Mifumo ya kutambua na kuthibitisha data za maumbile zimetumika kwa zaidi ya miaka 25. Mbinu zinazotumika katika BVR hazina madhara yoyote ya kiafya.

Je, mahitaji yapi yafaa kutimizwa na mtu ili asajiliwe kwa kama mpiga kura kwa kutumia BVR?
Kusajiliwa kama mpiga kura unahitaji kufika mwenyewe katika kituo cha usajili ukiandamana na stakabadhi zifuatazo za kujitambulisha;

a) Kitambulisho cha kitaifa ama
b) Pasipoti

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *