MASWALI ya Usaili Ajira za Jeshi la Polisi

MASWALI ya Usaili Ajira za Jeshi la Polisi
MASWALI ya Usaili Ajira za Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi amewatangazia vijana walioomba ajira ya Jeshi la Polisi
kupitia mfumo wa Ajira (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL) kuwa usaili utafanyika kuanzia tarehe 28/4/2025 saa 07:00 asubuhi hadi tarehe 11/5/2025 kote nchini.
Kuelekea usaili huo, haya hapa ni baadhi ya maswali ya kawaida yanayoulizwa mara Kwa mara kwenye usaili wa ajira za Jeshi la Polisi Tanzania pamoja na Majibu yake.
MASWALI YA USAILI WA JESHI LA POLISI
Tueleze Kuhusu Wewe
Eelezea jina lako, elimu yako, historia ya kazi (kama ipo), na sababu ya kutaka kujiunga na Jeshi la Polisi.
Mfano “Mimi naitwa Daud Adam, nimemaliza kidato cha sita mwaka 2024, ninaipenda kazi ya polisi kwa sababu natamani kulinda usalama wa raia na mali zao.”
Kwa nini unataka kujiunga na Jeshi la Polisi?
Eleza nia yako ya kutoa huduma kwa jamii, kulinda raia, kupambana na uhalifu, n.k, Katika Swali epuka kusema neno kwa sababu ya mshahara au ajira tu.
Majukumu ya Polisi ni yapi?
Kulinda amani na usalama, kutekeleza sheria, kupambana na uhalifu, kusaidia wakati wa majanga.
Kama ukipewa amri ambayo unaona haifai au si ya haki, utafanyaje?
Ningemjulisha afisa wa juu zaidi au kueleza kwa heshima sababu ya wasiwasi wangu kuhusu amri hiyo.
Changamoto gani unaifahamu katika Kazi ya Polisi?
Kukabiliana na wahalifu hatari, kazi ya muda mrefu, presha kubwa, lawama kutoka kwa jamii, lakini niko tayari kuzishughulikia.
Utafanya nini Wakati wa Matatizo au Presha Kubwa?
Napenda kutulia, kufikiria kwa makini kabla ya kuchukua hatua, na kushirikiana na wenzangu kutatua tatizo.
Umejiandaaje, kimwili na kiakili kwa kazi hii?
Eleza Mazoezi unayofanya, Nidhamu na Maadili yako.
Ukipewa Rushwa utafanyaje?
Sitakubali rushwa kwa sababu ni Kinyume cha Maadili na Sheria.
Hapa chini tumekuwekea Maswali tu ambayo unapaswa kuyafanyia Kazi Kwa kutafuta majibu yake kwani ni maswali ambayo unaweza kukutana nayo.
- Nani Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania kwa sasa?
- Eleza Sifa Kuu za Askari Mzuri wa Polisi.
- Una Maoni gani kuhusu hali ya Usalama nchini kwa sasa?
- Unaamini unaweza kufanya kazi katika mazingira yoyote?
- Kwa nini unataka kujiunga na Jeshi la Polisi?
- Unafahamu nini kuhusu Jeshi la Polisi Tanzania?
- Eleza historia Fupi ya Jeshi la Polisi Tanzania.
- Unaelewa nini kuhusu nidhamu ya kijeshi?
- Ukikosea ukiwa kazini, utachukua hatua gani?
- Umewahi kushiriki au kuhukumiwa kwenye kosa lolote la jinai?
- Unaweza kufanyia kazi mkoa wowote nchini?
- Eleza maana ya Utiifu kwa Mamlaka.
- Unadhani ni changamoto gani kubwa inayolikabili Jeshi la Polisi kwa sasa?
- Uzalendo ni nini
- Andika Nyimbo ya Taifa
- Taja Makujuku ya Polisi Wakati wa Uchaguzi
- Taja vyeo ya polisi Tanzania
- Taja Sheria Kuu inayoliongoza Jeshi la Polisi Tanzania.
- Eleza maana ya “kuzuia uhalifu” kwa kutumia mfano.
- Ni adhabu gani mtu hupata kwa kosa la wizi wa kutumia silaha?
- Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianza kutumika lini?
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nani?
- Eleza majukumu ya Polisi kulingana na Katiba.
- Eleza maana ya haki za Binadamu.
- Nini maana ya Amri halali na amri haramu?
- Itaje Mikoa yote ya Tanzania.
- Tanzania ina Majimbo/Mikoa mingapi ya Uchaguzi kwa sasa?
- Waziri gani anayesimamia masuala ya Mambo ya ndani ya Nchi?
- Eleza hatua za kumkamata mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria.
- Ungekuwa Askari na ukashuhudia Askari mwenzako anakiuka sheria ungefanyaje?
- Uhuru wa Tanganyika ulipatikana mwaka gani?
- Kama Askari Polisi, utachukua hatua gani kukabiliana na uhalifu wa mitandaoni?
- Eleza utaratibu wa kutoa taarifa ya tukio la jinai kwa Polisi.
- 33.Unaumwa ugonjwa wowote sugu?
- Uko tayari kuishi mbali na familia kwa muda mrefu kwaajili ya kazi?
- Unadhani unakidhi vigezo vya afya na nguvu kwaajili ya kazi ya Kipolisi?
- Ungewezaje kushughulikia maandamano yasiyo halali?
- Je, uko tayari kufanya Mazoezi ya kijeshi kila siku?
Hapa chini tumekuwekea baadhi ya Maswali ambayo watu wengine wamefanya kwenye saili zilizopita.
MIMI NIMESHAFANYA USAILI NIKAKOSA, volume ya watu ilikuwa kubwa sana especially kwenye course yangu na zingine (clinical medicine) Tulianza kwa kupangwa kicourse then tukaanza usaili wa fitness kuzunguka uwanja round 20, then tukaenda kuchek afya vipimo vyote tulilipia elfu 10k kila mmoja, then kuchunguliwa kama kawaida, unaingizwa kwenye chumba unavua nguo zote wanakukagua, mwili mzima, tatoo, deformity yoyote pamoja na meno na kinywa.
Then tukamalizia na mtihan ambao tulifanya written na OSCE kwa sisi madaktari unakuta upepangiwa vifaa mbali mbali vya afya na namba zake unachagua namba then maswali yanaanza, baada ya hapo tukamaliza tukaambiwa tutapewa majibu.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Hi hay naswali unakuwa unaulizwa kwa kiengereza au
Duuh
Ndyo
Good question
Sema nn? Ya mungu mengii