MASWALI ya Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA

MASWALI ya Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA
MASWALI ya Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza Matokeo ya usaili wa kuandika 2025 ambapo inatarajiwa kuendesha Usaili wa vitendo kwa nafasi za Madereva na Waandishi Waendesha Ofisi kuanzia tarehe 2 hadi 4 Mei, 2025 ambao utafuatiwa na usaili wa mahojiano unaotegemea kufanyika kwa kuanzia tarehe 7 hadi 9 Mei, 2025.
Kuelekea usaili huo, haya hapa ni baadhi ya maswali ya mahojiano (oral interview) pamoja na maswali ya vitendo (practical interview) hasa kwa nafasi kama ya Tax Officer, Customs Officer, au nafasi nyingine za kiutawala TRA.
Aidha Maswali ya usaili wa mahojiano na vitendo TRA yamegawanywa katika makundi mawili kama inavyoonekana hapa chini.
A. Maswali ya Usaili wa Mahojiano (Oral Interview), Haya ni maswali ya ana kwa ana, yakikujaribu katika ujuzi wa jumla, taaluma na maadili kazini:
Maswali yake yanaweza kuwa Katika Mfumo ufuatao.
- Tueleze kwa kifupi kuhusu wewe.
- Kwa nini unataka kufanya kazi TRA?
- TRA ni taasisi ya aina gani, na majukumu yake ni yapi?
- Tofautisha kati ya kodi ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja.
- Unafahamu nini kuhusu sheria ya kodi ya mapato (Income Tax Act)?
- Ni changamoto gani zinazoikumba TRA katika ukusanyaji wa kodi
- Ungewezaje kushughulikia mlipakodi anayekataa kulipa kodi
- Ni vigezo gani vinatumika kukokotoa VAT?
- Kodi ni nini? na ni kwanini wananchi watoe kodi?
- Taja aina kuu za kodi unazozifahamu.
B. Maswali ya Usaili wa Vitendo (Practical Interview), Hapa hujaribiwa uwezo wako wa kiutendaji, kuandika, kukokotoa, kutumia kompyuta na kuendesha gari Kutoka nafasi uliyoiomba.
Maswali ya Vitendo – Tax Officer / Accountant / Auditor yanaweza kuwa Katika mfumo huu.
Kokotoa kodi ifuatayo:
Faida kabla ya kodi = Tsh 120,000,000
Kiwango cha kodi ya kampuni = 30%
Swali: Kodi ya kulipa ni kiasi gani?
Jibu: Tsh 36,000,000)
- Andika barua ya kumbukumbu ya TRA kwenda kwa mlipakodi anayekwepa kodi.
- Jaza fomu ya VAT Return (kwa kutumia mfano wa takwimu walizokupa).
- Fafanua hatua za ukaguzi wa mlipakodi (Tax Audit Process).
- Tafsiri kifungu cha sheria ya VAT au Income Tax Act.
Maswali ya Vitendo – Customs Officer yanaweza kuwa Katika mfumo huu.
Kokotoa Ushuru wa Forodha:
CIF ya bidhaa = USD 10,000
Ushuru wa Forodha = 25%
VAT = 18%
Swali: Jumla ya kodi inayolipwa ni kiasi gani?
- Fafanua mchakato wa kuingiza bidhaa bandarini hadi zifikie sokoni.
- Tambua nyaraka za lazima katika uingizaji bidhaa (e.g. Bill of Lading, Invoice, Packing List).
Maswali ya Vitendo – IT Officer / Admin yanaweza kuwa Katika mfumo huu.
- Tengeneza taarifa kwa kutumia Excel (mfano: payroll ya wafanyakazi 10).
- Andika memo ya kiutendaji kwa Meneja.
- Jibu maswali ya matumizi ya mfumo wa TRA (e.g. TANCIS, eFiling).
- Maswali ya kujua MS Word, Excel, na Email etiquette.
Ili Kufuzu Katika Usaili wa Mahojiano na Vitendo TRA hakikisha umepitia maswali yote yanayoweza kuulizwa Wakati wa Usaili.
Maswali mengine zaidi bofya hapa
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
