Matokeo Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi Msimu wa December 2024
Matokeo Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi Msimu wa December 2024Matokeo Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi Msimu wa December 2024.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linapenda kuufahamisha umma kuwa limeidhinisha matokeo ya Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi katika ngazi ya I, II na III iliyofanyika mwezi December, 2024.
Mitihani hiyo iliratibiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
Jumla ya watahiniwa 41,331 walifanya mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi ambapo wasichana ni 14,215 sawa na asilimia 34.4 na wavulana 27,116 sawa na asilimia 65.6.
Matokeo ya Mitihani Kati ya watahiniwa 41,331 waliofanya mitihani, watahiniwa 35,355 sawa na asilimia 86 wamefaulu.
Watahiniwa 5,976 sawa na asilimia 14 wanapaswa kurudia mitihani yao.
Matokeo ya mitihani hiyo ni katika fani za Ufundi Magari, Ufundi Umeme, Ushonaji, Uchapaji, Usindikaji Vyakula, Huduma za Biashara, Kilimo, Madini, Ukarimu na Utalii pamoja na Urembo.
Kufutiwa matokeo hayo Watahiniwa wawili (2) wamefutiwa matokeo yao kutokana na ukiukwaji wa taratibu za mitihani.
Kupata matokeo ya mitihani ya CBA, Uanagenzi na NABE kwa msimu wa Desemba, 2024 bonyeza link hapa chini.
TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA UFUNDI STADI MSIMU WA DESEMBA 2024 |
---|
Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe: dac@veta.go.tz na namba ya simu 0755267489.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Matokeo Mitihani ya Taifa ya Ufundi Stadi Msimu wa December 2024