MATOKEO Simba vs RS Berkane 25 May 2025

MATOKEO Simba vs RS Berkane 25 May 2025
MATOKEO Simba vs RS Berkane 25 May 2025
Klabu ya Simba SC imeambulia sare ya bao 1-1 na RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa Pili wa Fainali ya CAF Confederation Cup 2024/2025 uliofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Matokeo hayo yanaifanya RS Berkane kutwaa taji la CAF Confederation Cup kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane.
Bao la Simba kwenye mchezo wa Leo lilifungwa na Joshua Mutale Katika dakika ya 17 huku la RS Berkane likifungwa Sidibe dakika ya 90’+3.
Huu unakuwa ubingwa wa tatu kwa RSB Berkane baada ya kutwaa taji hilo mwaka 2020 na 2022, mwaka ambao pia walitwaa taji la CAF Super Cup.
Kwa Simba SC imekuwa mara ya pili wanamalizia nyumbani Fainali za CAF na kushindwa kutwaa taji baada ya mwaka 1993 pia kufungwa 2 – 0 na Stella Adjame ya Ivory Coast Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam kufuatia kutoa sare ya bila mabao awali Jijini Abidjan.
Pamoja na kupewa Kombe jipya, RS Berkane wanapatiwa kitita cha Dola za Kimarekani Milioni 2, huku washindi wa pili, Simba SC wakipata Dola Milioni 1.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
