Mchakato wa Kuchunguza na Kugawa au Kubadili Majina ya Majimbo ya Uchaguzi

Filed in Habari by on February 26, 2025 0 Comments
     
Mchakato wa Kuchunguza na Kugawa au Kubadili Majina ya Majimbo ya Uchaguzi

Mchakato wa Kuchunguza na Kugawa au Kubadili Majina ya Majimbo ya Uchaguzi

Mchakato wa Kuchunguza na Kugawa au Kubadili Majina ya Majimbo ya Uchaguzi

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TANGAZO KWA UMMA KUHUSU KUANZA KWA MCHAKATO WA KUCHUNGUZA NA KUGAWA AU KUBADILI MAJINA YA MAJIMBO YA UCHAGUZI KATIKA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inautangazia umma kuwa, mchakato wa kupokea mapendekezo ya kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi utafanyika kuanzia tarehe 27 Februari, 2025 hadi tarehe 26 Machi, 2025.

Tume inatekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia masharti ya ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, ambayo inaipa mamlaka ya kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika majimbo ya uchaguzi.

Kanuni ya Jukumu hilo pia linatekelezwa kwa kuzingatia masharti 18(1) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024. Mapendekezo ya kugawanywa au kubadilishwa kwa majina ya majimbo yawasilishwe Tume kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa katika kanuni ya 18(3) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, kama ifuatavyo:-

  • Mapendekezo yawasilishwe na kujadiliwa katika vikao vya
    halmashauri;
  • Mapendekezo yajadiliwe katika Kamati ya Ushauri ya Wilaya;
  • Mapendekezo yawasilishwe kwa Katibu Tawala wa Mkoa kwaajili ya kujadiliwa katika Kamati ya Ushauri ya Mkoa; na
  • Katibu Tawala wa Mkoa awasilishe

Tume mapendekezo yaliyopitishwa na kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa pamoja na viambatisho vifuatavyo:-

  • Muhtasari wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa;
  • Muhtasari wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya; na
  • Muhtasari wa Kikao cha Baraza la Madiwani.

Vigezo vitakavyotumika katika kugawanya majimbo ni kama ifuatavyo:-

  • Wastani wa idadi ya watu, ambapo kwa majimbo ya mjini ni kuanzia wastani wa watu 600,000 na majimbo ya vijijini ni kuanzia wastani wa watu 400,000;
  • Hali ya kiuchumi ya Jimbo;
  • Ukubwa wa eneo la Jimbo husika;
  • Mipaka ya kiutawala;
  • Jimbo moja kutokuwa ndani ya wilaya au halmashauri mbili;
  • Mpangilio wa maeneo ya makazi ya watu yaliyopo;
  • Uwezo wa ukumbi wa bunge;
  • Idadi ya Wabunge wa Viti Maalum Wanawake;
  • Upatikanaji wa njia za mawasiliano; na
  • Hali ya kijiografia ya eneo linalokusudiwa kugawanywa.

Maombi yote yawasilishwe kupitia anuani ifuatayo:-
Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Uchaguzi House, Eneo la Uwekezaji Njedengwa, Kitalu D, Kiwanja Na.4,
5 Barabara ya Uchaguzi,
S.L.P. 358,
41107 DODOMA.

Aidha, maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe 26 Machi, 2025
hayatofanyiwa kazi.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *