Mfano wa Barua ya Kuomba Ajira za Walimu

Mfano wa Barua ya Kuomba Ajira za Walimu
Mfano wa Barua ya Kuomba Ajira za Walimu
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ametangaza nafasi mpya za Ajira za Walimu mwaka 2025.
Katibu huyo amekaribisha Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi hizo kama ilivyoainishwa katika
tangazo hili. Ajira Mpya 1571 za Walimu MDAs & LGAs
Kutokana na Tangazo hilo la Ajira za Walimu 2025, hii hapa Mfano wa Barua ya Maombi ya Ajira Za Walimu Kupitia (UTUMISHI).
Moja ya vitu vya msingi mwombaji wa Ajira ya Walimu ni kuzingatia katika uandishi wa Barua ya kuomba kazi.
Hii hapa ni mfano wa muundo sahihi juu ya uandishi wa Barua ya Maombi ya kazi ya walimu 2024/2025.
Mambo ya Msingi katika Uandishi wa Barua ya Ajira ya Walimu 2025 ni kama ifuatavyo;
- Anwani ya mwandishi
- Anwani ya mwandikiwa
- Kichwa Cha Barua(dhumuni mahususi)
- Shina la barua, hapa utaandika kulingana na kichwa Cha Barua, ukigusia jina lako,umri, kiwango chako Cha elimu na uzoefu wako kwa kifupi zaidi.
Ili kuandika barua nzuri ya maombi ya Ajira za Walimu, anza kwa kuweka mapendeleo ya salamu na utangulizi.
Hapa ni mfano wa barua ya kuomba ajira za ualimu:
Jina lako
Anwani yako
Simu yako
Barua pepe yako(email)
Tarehe
Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu
(Chuo/Shule/Jina la Taasisi)
(Anwani ya Taasisi)
YAH: MAOMBI YA AJIRA YA UALIMU
Nashukuru kwa nafasi ya kuwasilisha maombi yangu ya kazi ya ualimu katika taasisi yenu. Mimi ni (Jina lako kamili), na ni mtaalamu mwenye shahada ya (shahada yako) kutoka (jina la chuo). Pia, nina uzoefu wa kufanya kazi kama mwalimu wa (somo lako) kwa zaidi ya (miaka ya uzoefu).
Kwa sasa, napenda kujiunga na timu yenu na kutoa mchango wangu katika kuboresha elimu ya wanafunzi, nina ujuzi mzuri katika kufundisha, kupanga na kutekeleza mipango ya masomo, na pia nina uwezo wa kushirikiana vyema na wanafunzi.
Ningependa kuwa na nafasi ya kuzungumza nanyi kwa undani zaidi kuhusu jinsi ambavyo naweza kuleta mchango mkubwa kwa shule hii.
Nashukuru kwa muda wenu na ninatarajia majibu kutoka kwenu.
Wako Mtiifu
Signature yako
Jina lako kamili

Mfano wa Barua ya Kuomba Ajira za Walimu
Aidha huu ni mfano wa barua ya kuomba ajira za ualimu, hivo unaweza kubadilisha sehemu yoyote kulingana na hali yako au maelekezo ya taasisi unayoiomba Ajira.
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
