Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Filed in Makala by on February 13, 2025 1 Comment
     
Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa mamlaka aliyopewa Kwa mujibu wa kifungu cha 14(4) cha Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 5(1) ya kanuni za Utumishi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji za mwaka 2008 ametangaza nafasi za ajira ngazi ya Konstebo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa vijana wenye sifa zifuatazo Katika Tangazo la Ajira lifuatalo…..Ajira Mpya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Kutokana na Tangazo hilo hapa chini tumekuandalia mfano wa barua ya maombi ya kazi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Endapo wewe una sifa zilizoainishwa Katika Tangazo hilo fuata Maelekezo haya kuandaa barua yako kwaajili ya Maombi hayo.

(Jina Lako)
(anuani yako)
(tarehe)

Kamanda Mkuu
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
(Anuani ya Jeshi la Zimamoto)

YAH: MAOMBI YA KAZI KATIKA JESHI LA ZIMAMOTO

Nashukuru kwa muda wenu wa kuisoma barua yangu. Mimi ni (jina lako), ni mtaalamu katika [elimu yako) na naomba kuwasilisha maombi yangu ya kujiunga na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kama (jina la cheo au nafasi inayotaka).

Nina sifa na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya hatarishi na ya changamoto, ikiwa ni pamoja na uwezo wangu wa kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzangu, na kujitolea ili kuokoa maisha ya watu na mali zao. Nimepata mafunzo katika (eleza masomo au mafunzo ya awali, kama vile mafunzo ya afya, usalama, uokoaji, n.k.), ambayo ni muhimu kwa nafasi hii.

Pia, sina rekodi ya makosa ya sheria na ni mtu anayeweza kutii na kufanya kazi kwa bidii. Ninatarajia kuwa sehemu ya timu ya Jeshi la Zimamoto na kutoa mchango wangu kwa jamii.

Pamoja na barua hii nimeambatanisha vivuli vya vyeti vyangu vya taaluma na mahitaji mengine yote kwa mujibu wa tangazo vitu vimeambatanishwa kwenye mfumo.

Naomba kupata fursa ya kujitambulisha zaidi na kutoa maelezo ya kina kuhusu uzoefu wangu na sifa zangu. Nitafurahi kuwa na mahojiano kwa njia yoyote itakayowezekana.

Nashukuru kwa kuzingatia ombi langu.

Wako kwa dhati,

(Signature yako)
(Jina Lako)
(Simu yako)
(email/barua pepe yako)

Zingatia huu ni mfano ya maombi ya kazi katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Hivo hakikisha unaondoa au kubadilisha sehemu zinazohitaji uboreshaji kulingana na uhitaji wako.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Comments (1)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Yohana simoni bakari says:

    Nahitaj matangazo ya kazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *