MULEBA DC Yanunua Boti MV Muleba

Filed in Habari by on May 14, 2025 0 Comments
     
MULEBA DC Yanunua Boti MV Muleba

MULEBA DC Yanunua Boti MV Muleba

MULEBA DC Yanunua Boti MV Muleba

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba imechukua hatua kubwa kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa visiwa 39 vilivyopo Ziwa Victoria kwa kununua boti mpya ya abiria yenye uwezo wa kubeba watu 27 kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 268.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa boti hiyo katika mwalo wa Kyamkwikwi, Kata ya Izigo, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Dkt. Abel Nyamahanga amesema kuwa chombo hicho kitawezesha wakazi wa visiwani, wakiwemo wagonjwa wanaopata rufaa, kufika kwa urahisi hospitali zilizoko nchi kavu.

MULEBA DC Yanunua Boti MV Muleba

MULEBA DC Yanunua Boti MV Muleba

“Boti hii ni muhimu sana kwa ajili ya kurahisisha usafiri na pia kuboresha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wakazi wa visiwa hivi. Pia itasaidia viongozi wa Serikali kuwafikia wananchi kwa haraka na ufanisi zaidi,” alisema Dkt. Nyamahanga.

Amesisitiza kuwa chombo hicho kinapaswa kutumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kiwe na manufaa ya muda mrefu.

Kwa mujibu wa Bw. Evart Kagaruki, Afisa Mipango wa Halmashauri, Serikali Kuu ilitoa shilingi milioni 300 kufanikisha mradi huo. Kiasi kilichobaki, shilingi milioni 31, kitatumika kununua boti ndogo kwaajili ya shughuli za doria kwenye visiwa hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhe. Magongo Justus, ameeleza kuwa hapo awali usafiri ulikuwa wa mashaka hasa wakati wa hali mbaya ya hewa, hivyo ujio wa boti hiyo ni suluhisho la kudumu kwa changamoto hiyo.

Aidha, Mhe. Magongo ameleza kuwa Halmashauri inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu la Muleba, miradi ya afya, elimu na mingine mingi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!