MWONGOZO wa Walimu wa Kujitolea

MWONGOZO wa Walimu wa Kujitolea
MWONGOZO wa Walimu wa Kujitolea
Mwongozo wa Walimu wa Kujitolea Katika Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari Nlna Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi Tanzania Bara.
Mwongozo wa Walimu wa Kujitolea umeandaliwa ili kutoa maelekezo ya namna ya kupata walimu wenye sifa stahiki na kuwaajiri kwa mkataba wa kujitolea, kutoa taratibu za mafunzo kabilishi, kupanga na kutoa maelekezo ya kutosha kitaaluma na kitaalamu ili kazi zifanyike kwa ufanisi.
Aidha, Mwongozo huu unalenga kutoa maelekezo ya upatikanaji wa walimu wanaojitolea na huduma zao ikiwemo: posho, motisha na usimamizi wa nidhamu pahala pa kazi kwa kuzingatia masharti ya ajira za mkataba.
Inatarajiwa kuwa matumizi ya Mwongozo huu yataimarisha ushirikiano wa wadau wa elimu hususani Uongozi wa Elimu, jamii, walimu na wazazi.
Pia Mwongozo utawezesha walimu wanaojitolea kutoa huduma stahiki za ujifunzaji na ufundishaji kwa kuzingatia matakwa ya elimu nchini.
Hii itasaidia kutatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji na kuleta matokeo chanya yaliyokusudiwa katika Elimu ya awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MWONGOZO WA WALIMU WA KUJITOLEA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Mwongozo ni mzuri, lakini sawali langu ni je, huyu mwalimu wa kujitolea atajitolea mpaka lini ndio aajiriwe?
Na mbona hakuna kipengele chochote cha kutoa kipaumbele kwa ajira ya kudumu kwa mwalimu wa kujitolea?