NACTVET yazindua Kampeni ya Mwanachuo Smart

NACTVET yazindua Kampeni ya Mwanachuo Smart
NACTVET yazindua Kampeni ya Mwanachuo Smart, Mwanachuo Smart Jihudumie Popote.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limezindua kampeni ya Mwanachuo Smart yenye lengo la kukuza uelewa wa wanachuo wa ngazi ya Astashahada na Stashahada kuhusu mifumo mbalimbali ya kidigitali ya NACTVET kwaajili ya kujipatia huduma mbalimbali.
Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi tarehe 6 Mei, 2025 na Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda na kuhudhuriwa na viongozi wa TAHLISO pamoja na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
Miongoni mwa mifumo mahsusi kwaajili ya kuhudumia wanafunzi ni Mfumo wa Kuhakiki Udahili wa Wanafunzi (Student Information Verification), Mfumo wa kuomba Namba ya Utambuzi wa Tuzo (AVN) na Mfumo wa kuomba Hati ya Matokeo (Transcript) ambayo inapatikana kupitia tovuti ya www.nactvet.go.tz.
Mifumo hiyo inaweza kutumiwa na wanafunzi kwa urahisi popote pale walipo bila ulazima wa wao kufika kwenye ofisi za NACTVET.
Katika kampeni hiyo, NACTVET itashirikiana kwa karibu na viongozi wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu nchini (TAHLISO) kutoa elimu kwenye vyuo mbalimbali pamoja na kuandaa maudhui kuhusu matumizi ya mifumo hiyo na kusambaza kwa wanafunzi kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha, vyuo mbalimbali vitatembelewa ambapo NACTVET itatoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kuwaelekeza namna ya kutumia mifumo hiyo.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
