NAFASI 12 Za Kazi Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili

NAFASI 12 Za Kazi Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
NAFASI 12 Za Kazi Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Mradi wa Kinga na Matumaini (PRE-HOPE) Study: Nafasi 12 Mpya za Kazi Februari, 2025
Maelezo ya Kazi
Fursa za Kazi kwenye Utafiti wa ‘Kinga na Matumaini (PRE-HOPE)’: Mradi huu wa Utafiti wa Kinga na Matumaini ni wa miaka mitatu (3) wenye lengo la kuboresha matumizi ya Dawa kinga ya VVU (PrEP) miongoni mwa wanawake wanaotumia dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.
Mradi huu utatumia njia ya Mahojiano ya Motisha kwa matumizi ya Dawa-Kinga ya VVU, pamoja na kuunganisha Mbinu za Matibabu ya Kisaikolojia yenye Vipengele mbalimbali na Mahojiano ya Motisha kwa matumizi ya Dawa-Kinga ya VVU ile kuuweza kutolewa na watoa huduma za wasiowataalam (“Paraprofessionals”).
Madhumuni ni kuboresha matumizi ya Dawa kinga ya VVU miongoni mwa wanawake wanaotumia dawa za kulevya.
Baada ya hapo, kutakuwa na tathmini ya awali kwa washiriki 200 WWUD yatakayopima uwezekano (“feasibility”), uaminifu (“fidelity”) na ufanisi wa awali (“Preliminary efficacy”) wa mbinu hizi.
Kwa sasa tunatafuta watoa huduma wasio wataalamu na wasaidizi wa Utafiti
(Reserch Assistants) wenye shauku na ari ya kushiriki katika mradi huu muhimu.
Fursa za Kazi katika Mradi wa Utafiti: ‘Prevention and Hope (PRE-HOPE)/Kinga na Matumaini’
Orodha ya Kazi:
Washauri wa Afua (Intervention Counselors) (Nafasi 10)
Kituo cha Kazi: Dar es Salaam
Tarehe Inayotarajiwa ya Kuanza: 17 Machi 2025
Majukumu ya Msingi:
- Kutoa ushauri wa afya ya akili kwa kutumia mbinu za Matibabu ya Kisaikolojia yenye Vipengele
mbalimbali ama “CETA=Common Elements Treatment Approach” kwa wanawake wanaotumia
dawa za kulevya. - Kushiriki mafunzo ya awali na endelevu juu ya utoaji wa huduma za CETA, ikijumuisha mafunzo
ya lazima ya siku 10 pamoja na vikao vya usimamizi (supervision) vya kila wiki vya masaa 1-3. - Kutoa msaada wa kisaikolojia na ushauri wa kupunguza matumizi ya dawa za kulevya kwa
kuzingatia miongozo ya mradi. - Kushiriki katika ufuatiliaji na kuwatafuta washiriki katika jamii (community tracing) ili kuimarisha
ushiriki wao katika CETA na katika utafiti. - Kuhifadhi kumbukumbu sahihi za vikao vya ushauri, zikiwemo fomu za ufuatiliaji wa washiriki na
nyaraka za ufuatiliaji wote uliofanyika. - Kushirikiana na wasimamizi na timu ya utafiti katika kupata mrejesho, ushauri endelevu na
kuzingatia taratibu zilizowekwa (protocol adherence). - Kuwaunganisha washiriki katika huduma zinazostahili pale inapohitajika, ikiwemo msaada kwa
wahanga, msaada wa vitendo dhidi ya ukatili wa kijinsia au huduma za tiba. - Kuripoti mara moja masuala yote ya kiusalama kama mawazo ya kujiua, ukatili wa majumbani, au unyanyasaji wa watoto kwa wasimamizi na mamlaka zinazohusika.
Sifa Zinazohitajika (Qualifications):
- Angalau Cheti cha Shule ya Sekondari (Kidato cha Nne) au zaidi; mafunzo ya ziada katika ushauri, afya ya jamii, au nyanja zinazohusiana ni faida.
- Uzoefu kama mshauri wa watoa elimu rika kuhusu VVU, mshauri wa kisaikolojia, au kazi za afya
ya akili katika jamii ni kipaumbele. - Uelewa wa msingi wa misingi ya ushauri, msaada wa kijamii, na kanuni za usiri.
- Uwezo mzuri wa mawasiliano na uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea kwenye maeneo ya
jamii. - Kujitolea kushiriki mafunzo na usimamizi kama inavyoelekezwa na utafiti.
- Uzoefu wa kufanya kazi na jamii zilizotengwa, hususan watu wanaotumia dawa za kulevya au
wenye changamoto za afya ya akili. - Ujuzi wa taratibu za huduma za VVU katika vituo vya serikali au afya ya umma ni nyongeza nzuri.
- Uwezo wa kuzungumza na kuandika lugha ya Kiswahili kwa ufasaha.
✅Wasaidizi wa Utafiti (Nafasi 2)
Kituo cha Kazi: Dar es Salaam
Tarehe Inayotarajiwa ya Kuanza: 17 Machi 2025
Majukumu Muhimu
- Kukusanya data za msingi na za ufuatiliaji (dodoso zilizoundwa, mahojiano ya kina, mikutano ya
vikundi focus group discussions) na kuhakikisha kufuata kanuni za maadili ya utafiti na taratibu za
kazi (SOPs). - Kufanya kazi moja kwa moja na wanawake wanaotumia dawa za kulevya , kukusanya taarifa juu
ya matumizi ya PrEP, afya ya akili, na tabia za matumizi ya dawa za kulevya. - Kupata ridhaa ya washiriki, kusaidia katika uchunguzi na usajili wa washiriki, na kutambulisha
utafiti kwa WWUD kwa ajili ya kuthibitisha sifa za kujiunga . - Kuratibu upimaji wa VVU katika vituo vinavyoshirikiana na kuhakikisha majibu hasi ya VVU
(HIV-negative test results) yanathibitishwa kabla ya usajili. - Kuingiza, kunukuu (transcribe), na kuhakiki data za kitabiti na kishirika kwa kutumia REDCap, au NVivo, huku ukizingatia usiri mkali.
- Kutunza kumbukumbu safi na za siri za uchunguzi, usajili, na tathmini za washiriki (tathmini ya
afya ya akili, dodoso za tabia). - Kufuatilia maendeleo ya washiriki, kurekodi changamoto au mabadiliko yoyote uwanjani, na kuripoti wasiwasi wowote kwa timu ya utafiti.
- Kuendana na ratiba za washiriki (mchana au jioni) ili kuhakikisha ubora wa juu wa ukusanyaji data
na ufuatiliaji endelevu. - Kushiriki katika mikutano ya timu ya utafiti na mafunzo, na kuingiza mrejesho katika taratibu za
ukusanyaji data. - Kushirikiana na timu ya utafiti ili kuhakikisha utekelezaji unaozingatia tamaduni za jamii na
kuweka viwango bora vya ubora wa data.
Sifa na Ujuzi (Qualifications & Skills):
- Shahada ya kwanza katika Tiba, Uuguzi, Afya ya Umma, Saikolojia, Sosholojia, Kazi za Jamii, au
fani inayohusiana. - Angalau mwaka mmoja wa uzoefu wa kufanya utafiti, hususan utafiti unaohusiana na masuala ya afya au jamii unaojumuisha Makundi Muhimu na Yaliyo katika Hali Hatarishi (KVP).
- Uzoefu katika mbinu za ukusanyaji data za kitakwimu na kimaelezo (quantitative and qualitative),
pamoja na utaalamu wa kunukuu na kufanyia msimbo data. - Ujuzi mzuri wa kompyuta, hasa katika uingizaji na usimamizi wa data (mfano NVivo, REDCap,
ODK). - Ufasaha katika kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingereza.
- Uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya jamii, ikiwa ni pamoja na yale yenye makundi
yaliyotengwa au yaliyo katika hatari. - Uzoefu wa kufanya mahojiano ya kina, mikutano ya vikundi au mahojiano na watu muhimu ni
faida ya ziada. - Ujuzi mzuri wa mawasiliano na ushirikiano, ukiwa na uwezo wa kujenga uhusiano mzuri na
makundi yaliyo hatarini. - Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea huku ukizingatia taratibu za utafiti na muda uliopangwa.
Masharti ya Maombi kwa Kazi Zote:
- CV yenye taarifa za mawasiliano (anwani ya posta, barua pepe, na namba ya simu).
- Nakala za vyeti muhimu (Shahada ya Uzamili/Shahada ya Kwanza, Stashahada, n.k.).
- Picha ndogo ya pasipoti na nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Nyaraka za kitaaluma zilizoidhinishwa pale inapohitajika.
- Wadhamini wawili wenye taarifa za mawasiliano.
- Uwasilishaji wa vyeti bandia vya kitaaluma na taarifa nyingine za uongo kwenye CV utasababisha
hatua za kisheria.
Ajira Mpya 12 Za Kazi Chuo Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Maulizo yanaweza kutumwa kwa Dkt. Sifaely Mtaita hadi tarehe 24 Februari, 2025 kwa namba ya simu: +255754398720.
Mshahara na Manufaa: Mshahara utazungumzwa wakati wa usaili.
Fursa za mafunzo endelevu na ushauri.
Jinsi ya Kutuma Maombi: Ikiwa una nia na unazo sifa zinazohitajika, tafadhali tuma Vyeti vyako vya Kitaaluma, barua ya maombi inayoeleza kwa nini wewe ni mwafaka kwa nafasi hii, pamoja na wasifu wako (CV) unaoeleza uzoefu wako na sehemu unayofanyia kazi kwa sasa kwenda kwa:
Mr Abbas Mkila amkila@muhas.ac.tz, Nakala kwa Dr. Sifaely Mtaita: sifaelabbie@gmail.com
Waombaji watakaofuzu katika mchujo ndio watataarifiwa tarehe ya usaili.
Tunahimiza maombi kutoka kwa
watu wenye uzoefu binafsi wa kutumia dawa za kulevya au wale waliowahi kufanya kazi na wanawake wanaotumia dawa za kulevya au Makundi Maalumu Yaliyo katika Hali Hatarishi ya kupata VVU (KVP).
Mwisho wa Kutuma Maombi: March 02, 2025.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: NAFASI 12 Za Kazi Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili