Nafasi 13 Za Afisa Fiziotherapia Wizara ya Afya

Filed in Ajira by on March 6, 2025 0 Comments
     
Nafasi 13 Za Afisa Fiziotherapia Wizara ya Afya

Nafasi 13 Za Afisa Fiziotherapia Wizara ya Afya

Nafasi 13 Za Afisa Fiziotherapia Wizara ya Afya

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Position: Afisa Fiziotherapia (Physiotherapy Officer II) – 13 Post

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kufanya kazi zote za Mfiziotherapia hospitalini zinazohusiana na
    magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, wazee,na
    wote waliolazwa.
  • Kuchunguza mgonjwa, kupanga matibabu kulingana na tatizo la
    mgonjwana kufuatilia hali ya mgonjwa husika.
  • Kutoa ushauri wa tiba na rufaa ya mgonjwa kwa kada nyingine za
    afya kulingana na tatizo la mgonjwa.
  • Kutoa na kusimamia elimu ya Fiziotherapia, Utengamao na tiba na kuboresha afya ya mwili na viungo katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
  • Kutoa Ushauri nasaha wa Utengamao kwa wagonjwa katika jamii (CBR).
  • Kutunza takwimu za wagonjwa wa Fiziotherapia na watu wenye
    ulemavuna kuzitumia kama ilivyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
  • Kutathimini huduma za Fiziotherapia na Utengamao katika eneo lake la kazi.
  • Kusimamia na kuelekeza watumishi walio chini yake.
  • Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za Fiziotherapia
    katikaeneo la kazi.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Fiziotherapia (BSc. in Physiotherapy) kutoka Vyuo Vikuu Vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili (Full Registration) kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Mishahara ya serikali TGHS C.

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi
    miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswakuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu
    walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed
    C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatuwa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za
    vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne,kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI – Computer Certificate – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
    matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
    vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
    NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
    kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia
    walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa
    kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140
    wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa
    hatua za kisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamojanavyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira portal (Recruitment Portal) kupitia anuani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 19 Machi, 2025.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!