Nafasi 1300 za Walimu Daraja La III C, Somo la Biashara

Filed in Ajira by on February 10, 2025 0 Comments
     
Nafasi 1300 za Walimu Daraja La III C, Somo la Biashara

Nafasi 1300 za Walimu Daraja La III C, Somo la Biashara

Nafasi 1300 za Walimu Daraja La III C, Somo la Biashara

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

MWALIMU DARAJA LA III C – SOMO LA BIASHARA (BUSINESS
STUDIES) NAFASI 1300 (LINARUDIWA)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kuandaa azimio la kazi, maandalio ya masomo, nukuu za masomo na
    Mpango wa Kazi wa majukumu mengine aliyokabidhiwa;
  • Kutengeneza na Kufaraghua zana za kufundishia na kujifunzia;
  • Kufundisha, kufanya Tathmini na kutunza kumbukumbu za Maendeleo ya Wanafunzi;
  • Kusimamia na kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi Shuleni na Darasani;
  • Kusimamia malezi ya wanafunzi Kiakili, Kimwili, Kiroho na kutoa ushauri nasaha na unasihi;
  • Kutoa ushauri wa Kitaalamu na kutaaluma kuhusu maendeleo ya Elimu;
  • Kusimamia na utunzaji wa vifaa na mali za Shule;
  • Kazi nyingine atakazopangwa na Mkuu wa Shule kulingana na majukumu ya Shule

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Elimu (Bachelor with Education) au Shahada
ya Ualimu (Bachelor of Education) yenye somo la kufundishia la Biashara au
Usimamizi wa Biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration
Business studies)

AU Shahada isiyo ya Ualimu/Elimu yenye somo la kufundishia la Biashara au usimamizi wa biashara (Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration na Business Studies) pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (Postgraduate Diploma in Education) kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vinavyotambulika na Serikali.

AU Wenye Shahada isiyo ya Ualimu katika fani ya Biashara/usimamizi wa
biashara/Commerce/ Bookkeeping/ Business Administration/Business
studies’’. waombaji ambao hawana somo la UALIMU ni lazima wawe tayari
kupata mafunzo ya UALIMU baada ya kuajiriwa.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGTS- D

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwaajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
    katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombiya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
    – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    – Computer Certificate
    – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa nakuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuombanisipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
    Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.

Maombi yoteyatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Februari, 2025

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *