NAFASI 17 Za Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wakina Mama MDAs & LGAs
NAFASI 17 Za Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wakina Mama MDAs & LGAs
✅DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA WAKINA MAMA (MEDICAL
SPECIALIST – GYNAECOLOGIST)- NAFASI -17
MAJUKUMU YA KAZI
- Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali katika fani husika.
- Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyo eneo lake la kazi.
- Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kutayarisha elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya.
- Kufundisha na kuelekeza watumishi walio chini yake.
- Kusimamia wafanyakazi walio chini yake Kubuni.
- Kuendesha na kutathimini utafiti na kusambaza matokeo.
- Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
- Kutoa huduma za outreach katika kanda.
- Kutoa huduma za medical legal
- Kushiriki katika kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa Sera na
Mipango ya Serikali juu ya afya. - Kushauri wizara kuhusu uendeshaji wa shughuli za afya nchini
- Kushiriki katika kamati ya jopo la madaktari (medical board) kwa ajiliya kustaafisha wafanyakazi kwa matatizo ya kiafya.
- Kutayarisha mitaala ya elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya.
xviii. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Uzamili ya Udaktari Bingwa au PhD kwenye fani ya
Udaktari wa Magonjwa ya akinamama kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali. Wawe wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali TGHS G.
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
- Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifakwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
– Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
– Computer Certificate
– Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards - “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
- Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 26 Juni 2025
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
Tags: NAFASI 17 Za Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wakina Mama MDAs & LGAs