Nafasi 37 Za Muuguzi Daraja la II Wizara ya Afya

Nafasi 37 Za Muuguzi Daraja la II Wizara ya Afya
Nafasi 37 Za Muuguzi Daraja la II Wizara ya Afya
Position: Muuguzi Daraja la II (Nurse II) Nafasi 37
Majukumu Ya Kazi
- Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya.
- Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu
yake ya kazi. - Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi.
- Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani.
- Kutoa ushauri nasaha.
- Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango.
- Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto.
- Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
- Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
Sifa za Mwombaji
Kuajiriwa wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo
kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za Mishahara ya Serikali TGHS A
MASHARTI YA JUMLA.
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi
miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini; - Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswakuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu
walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; - Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
Mwanasheria/Wakili. - Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed
C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatuwa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za
vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne,kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI – Computer Certificate – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards).
- “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. - Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
NACTE). - Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi
kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. - Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia
walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa
kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140
wa tarehe 30 Novemba, 2010. - Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa
hatua za kisheria.
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi
iliyosainiwa pamojanavyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe
kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa ajira portal (Recruitment Portal) kupitia anuani
ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/. (Anuani hii pia inapatikana
kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika
tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 19 Machi, 2025.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
