Nafasi 41 Fani ya Uhandisi na Udereva Ubungo Municipal Council

Filed in Ajira by on February 15, 2025 0 Comments
     
Nafasi 41 Fani ya Uhandisi na Udereva Ubungo Municipal Council

Nafasi 41 Fani ya Uhandisi na Udereva Ubungo Municipal Council

Nafasi 41 Fani ya Uhandisi na Udereva Ubungo Municipal Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo anapenda kuwatangazia Watanzania wote nafasi za kazi za mkataba katika fani ya Uhandisi na Udereva kwa mujibu wa kibali cha ajira ya mkataba chenye Kumb: Na. FA.97/228/02″A”/190 cha tarehe 19 Disemba, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Utumishi, hivyo kwa wale wenye sifa mnatakiwa kuomba nafasi hizi kama zilivyooanishwa kwa kuzingatia sifa tajwa:-

✅MHANDISHI MTENDAJI UJENZI II (EXECUTIVE CIVIL ENGINEER II) NAFASI (03)

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amefaulu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) wenye shahada (Degree) ya Uhandisi wa huduma za ujenzi kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali aliye sajiliwa na bodi ya usajili ya wahandisi kama professional engineer.

KAZI NA MAJUKUMU YA MHANDISI MTENDAJI UJENZI (EXECUTIVE CIVIL ENGINEER)

  • Kufanya ukaguzi wa barabara, Madaraja na Majengo mbalimbali.
    Kufuatilia utekelezaji wa sheria na kanuni za ujenzi wa barabara na majengo.
  • Kutayarisha bajeti ya mwaka ya ujenzi na matengenezo ya barabara, Madaraja na Majengo.
  • Kusimamia na kuratibu kazi za barabara/Madaraja na Majengo zinazotolewa na makandarasi.
  • Kutoa ushauri na usimamizi wa kazi za ujenzi wa miradi ya barabara/Madaraja na Majengo.
  • Kutayarisha taarifa za maendeleo ya miradi za mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima ili kueleza maendeleo ya kazi za ujenzi wa barabara, madaraja, nyumba ikijumuisha miradi iliyokamilika na inayoendelea.
  • Kusimamia utekelezaji wa sheria,kanuni za barabara/ Madaraja na Majengo na kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji.
  • Kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na majengo.
  • Kutayarisha taratibu za ununuzi na kuandaa mikataba kwaajili ya usanifu, ukarabati na kuinua viwango vya ujenzi wa barabara/ Madaraja na majengo.
  • Kutayarisha mipango ya mwaka pamoja na bajeti ya ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja na majengo.

NGAZI YA MSHAHARA: Mwombaji atakayefanikiwa kuajiriwa kwa cheo cha Mhandisi Mtendaji Ujenzi II atalipwa mshahara ngazi ya TGS E.1

✅MHANDISI UFUNDI NA UMEME II (MECHANICAL AND ELECTRICAL ENGINEER II) NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) Awe amehitimu mafunzo ya shahada katika fani ya Uhandisi Huduma za Umeme kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali aliye sajiliwa na bodi ya usajili ya wahandisi.

KAZI NA MAJUKUMU YA MHANDISI UFUNDI NA UMEME II (SERVICE ELECTRICAL ENGINEER II) NAFASI 1

  • Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomuhusu.
  • Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na mitambo mbalimbali, bei za magari na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi.
  • Kupitia mapendekezo ya miradi (Project Proposals) mbalimbali ya ufundi na umeme yanayowasilishwa wizarani.
  • Kuratibu miradi ya ufundi na umeme katika ngazi zote (Maandalizi, Ujenzi na Uendeshaji) na kutayarisha programu ya utekelezaji wa miradi hiiyo ya ufundi na umeme.
  • Kufuatilia maendeleo ya teknolojia mbalimbali ya ufundi na umeme kwa madhumuni ya kuboresha utaalamu huo kwenye fani hizi.
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi bora ya ufundi na umeme kutokana na maendeleo ya teknolojia, na matokeo ya utafiti na uvumbuzi yanayopatikana kwengineko.
  • Kufanya ukaguzi wa shughuli za ufundi na umeme ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora wa huduma zao.

NGAZI YA MSHAHARA: Mwombaji ataye fanikiwa kuajiriwa kwa cheo cha Mhandisi Huduma za Umeme II atalipwa mshahara ngazi ya TGS E.1

✅MHANDISI MAJENGO II (ARCHITECT II) NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) Awe amehitimu mafunzo ya Shahada katika fani ya Usanifu Majengo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali aliye sajiliwa na Bodi ya Usajili husika kama Professional Architect.

KAZI NA MAJUKUMU YA MSANIFU MAJENGO II (ARCHITECT II)

  • Kufuatilia upatikanaji wa taarifa na taaluma za usanifu wa majengo.
  • Kupitia mapendekezo ya miradi (Project Proprosals) mbalimbali ya majengo yanayowasilishwa wizarani.
  • Kuhakiki miradi ya majengo katika ngazi zote (Maandalizi, Ujenzi na Uendeshaji) na kutayarisha programu ya utekelezaji wa miradi hiyo.
  • Kufuatilia maendeleo ya wasanifu majengo mbalimbali na matokeo ya uvumbuzi na utafiti katika fani zao.
  • Kutoa ushauli wa kitaalamu kuhusu fani ya usanifu wa majengo kutokana na maendeleo ya teknolojia, na matokeo ya utafiti na uvumbuzi yapatikanayo kwingineko.
  • Kufanya ukaguzi wa majengo ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora wa majengo.

NGAZI YA MSHAHARA: Mwombaji ataye fanikiwa kuajiriwa kwa cheo cha Msanifu Majengo II atalipwa mshahara ngazi ya TGS E.1

✅MHANDISI MKADIRIAJI UJENZI II (QUANTITY SURVEYOR II) NAFASI 1

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) Awe amehitimu mafunzo ya shahada katika fani ya Ukadiriaji Ujenzi kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali aliye sajiliwa na Bodi ya Usajili husika kama Professional Quantity Surveyor.

KAZI NA MAJUKUMU YA MHANDISI MKADIRIAJI UJENZI II

  • Kuandaa mipango kazi na makisio ya gharama za ujenzi na zabuni (BOQ & Schedule of materials.
  • Kusaidia katika kufanya tathmini ya zabuni za miradi ya ujenzi.
  • Kupitia mapendekezo ya miradi (Project Proposals) mbali mbali ya majengo yanayowasilishwa wizarani na kutoa ushauri unaotakiwa.
  • Kusimamia mikataba ya ujenzi na kuhakikisha ubora na masharti yanatekelezwa.
  • Kusimamia na kufuatilia matumizi ya fedha na kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya bajeti.
  • Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi kutokana na maendeleo ya teknolojia, na matokeo ya utafiti na uvumbuzi yanayopatikana kwingineko.
  • Kufanya ukaguzi wa majengo ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora wa majengo.

NGAZI YA MSHAHARA: Mwombaji ataye fanikiwa kuajiriwa kwa cheo cha Mkadiriaji Ujenzi II atalipwa mshahara ngazi ya TGS E.1

✅DEREVA DARAJA II (NAFASI 35)

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe na cheti cha kidato cha nne (iv) au cha sita (vi)
  • Awe na leseni la daraja E au C1 yauendeshaji magari ambayo imefanyiwa kazi kwa muda usio pungua mwaka mmoja bila ya kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic driving course) yanayo tolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo kingine kinachotambuliwa na serikali.
  • Waombaji wenye cheti cha majaribio ya ufundi daraja la Il watafikiliwa kwanza.

KAZI NA MAJUKUMU YA DEREVA DARAJA LA II

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ilikubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
  • Kufanya usafi wa gari, na Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

NGAZI YA MSHAHARA: Mwombaji atakaye fanikiwa kuajiriwa kwa cheo cha dereva daraja la II atalipwa mshahara ngazi ya TGS B.1 kwa mwezi.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 -45.
  • Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa.
    Barua ya muombaji ioneshe anuani anayotumia kwasasa pamoja na namba ya simu ikiambatana na:-
  • Nakala za vyeti vya taaluma.
  • Nakala ya vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa na kazi husika.
  • Maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu zinazopatikana na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Picha mbili (2) za “Passport Size” za hivi karibuni.
  • Kitambulisho cha Taifa au namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
  • Waombaji waliowahi kupatikana na kosa la jinai maombi yao maombi yao hayatashughulikiwa.
  • “Testmonies”, “Provisional Result”, “Statement of results” hati ya matokeo ya Kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULT SLIPS HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa/ kuachishwa kazi katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama ana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Waombaji wenye sifa zaidi ya zilizotajwa hapo juu maombi yao hayatashughulikiwa.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi wa Manispaa,
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,
S.L.P 55068,
DAR ES SALAAM.

Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi wa Manispaa kwa anuani tajwa hapo juu kwa njia ya posta au kwakuleta ofisini moja kwa moja.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24 February, 2025.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *