Nafasi 50 Za Makarani wa Mapato Tanganyika District Council

Filed in Ajira by on March 3, 2025 3 Comments
     
Nafasi 50 Za Makarani wa Mapato Tanganyika District Council

Nafasi 50 Za Makarani wa Mapato Tanganyika District Council

Nafasi 50 Za Makarani wa Mapato Tanganyika District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika anawatangazia wananchi wote wenye sifa kuomba nafasi 50 za Makarani wa Mapato.

SIFA ZA KUAJIRIWA KWA MAKARANI WA MAPATO:
Waombaji wawe wamehitimu kudato cha nne waliofuzu na kutunukiwa vyeti vya mojawapo ya mafunzo ya Mgambo/JKT/Zimamoto ama mafunzo ya ulinzi wa Maliasili (VGS) kutoka katika Chuo kinachotambulika na serikali na kutunukiwa Vyeti. Mwombaji anaejua kutumia POS atakuwa na sifa ya nyongeza (ziada).

MAJUKUMU YA KAZI;

  • Kukusanya mapato katika maeneo (vizuizi/mageti) mbalimbali kwa kuzingatia vituo vilivyopangwa;
  • Kuwasilisha fedha zilizokusanywa kwa wakati kwa utaratibu maalumu uliowekwa;
  • Kuhakikisha magari na vyombo vya usafiri vinakaguliwa kujua kiasi cha mzigo kilichomo ili kujiridhisha endapo mazao/mzigo uliobebwa umelipwa ushuru sahihi.

Ngazi ya Mshahara; Maafikiano/ Majadiliano kati ya mwajiri na mwajiriwa kwa Kada husika.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI:

  • Mwombaji awe Raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45;
  • Mwombaji aambatishe nakala ya vyeti Elimu ya Sekondari, taaluma na nakala ya cheti cha
    kuzaliwa.
  • Waombaji watakaowasilisha “Result Slip, Statement of Results, Provisional Results au Transcripts” havitakubalika.
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (DetailCurriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji watakaowasilisha taarifa za kughushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi;
  • Mwombaji aambatishe picha ndogo (Passport size) mbili (2) kwenye barua ya maombi;
  • Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili;
  • Mwombaji aandike nje ya bahasha kazi/kada/nafasi anayoomba;
  • Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta hivyo, maombi yatakayowasilishwa kwa mkono hayatapokelewa;

Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa anuani ifuatayo:-

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,
S.L.P. 1,
MPANDA.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15.03.2025

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Comments (3)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Atupakisye mwakosya Rashid says:

    I need job

  2. Atupakisye mwakosya Rashid says:

    I graduate community development at cdti-mbeya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *