NAFASI 694 Za Walimu Wa Kujitolea Shule Za Msingi

Filed in Ajira by on May 17, 2025 2 Comments
     
NAFASI 694 Za Walimu Wa Kujitolea Shule Za Msingi

NAFASI 694 Za Walimu Wa Kujitolea Shule Za Msingi

NAFASI 694 Za Walimu Wa Kujitolea Shule Za Msingi Chini ya Mradi wa GPE – TSP

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mradi wa Kuboresha Kada ya Ualimu (Global Partnership for Education Teacher Support Programme – GPE – TSP) kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR TAMISEMI) inatekeleza afua mbalimbali ikiwemo ya kuratibu upatikanaji wa Walimu wa Kujitolea (engagement of volunteer teachers).

Mradi huu unatangaza nafasi za kujitolea kwa walimu 694 wa Shule za Msingi watakaofanya kazi chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa katika shule zenye uhitaji mkubwa zaidi kwa kuzingatia utaratibu wa kupanga walimu wa Shule za Msingi Primary Teacher Allocation protocol (P-TAP) ambao umeanishwa kwenye Andiko la Mradi huo wa GPE – TSP.

Hivyo, wahitimu kutoka Vyuo vya Ualimu na vinavyotambuliwa na Serikali wanatangaziwa kutuma maombi ya kujitolea katika Shule za Msingi mbalimbali kama zilivyoanishwa katika Mfumo wa ‘Online Teachers Application System (OTEAS)’ kuanzia tarehe 17 Mei – 30 Mei, 2025.

Nafasi zilizopo ni kwa wahitimu wa Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma).

TARATIBU ZA KUOMBA
Walimu wote wenye sifa watume maombi kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz. Tangazo hili linawahusu wahitimu wa Kozi za Ualimu kuanzia mwaka 2015 hadi mwaka 2023.

SIFA ZA KITAALUMA ZA MWOMBAJI
Walimu wanaoomba kujitolea katika Shule za Msingi wanatakiwa kuwa na sifa za kitaaluma kama ifuatavyo:

  • Mwalimu Daraja la III A – Mwenye Astashahada ya Ualimu Elimu ya Msingi (Certificate in Primary Education).
  • Mwalimu Daraja la III B Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Awali na
  • Mwalimu Daraja la III B Mwenye Stashahada (Diploma) ya Ualimu aliyesomea Elimu ya Msingi.

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe na umri usiozidi miaka 43;l.
  • Aambatishe nakala ya cheti cha Kuzaliwa, Kidato cha nne au sita, na Mafunzo ya Fani ya Ualimu.
  • Awe tayari kufanya kazi katika Shule za Msingi zenye mahitaji makubwa zaidi ya walimu wa kujitolea zilizopo pembezoni.
  • Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Taasisi nyingine.
  • Awe hajawahi kufukuzwa au kustaafishwa katika Utumishi wa Umma kwa makosa ya kiutumishi.
  • Awe na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA).
  • Waombaji waambatishe nyaraka zote muhimu katika mfumo na Waombaji wote waliosoma Elimu ya Sekondari nje ya nchi wanatakiwa kupata Namba ya Ulinganifu wa Matokeo (Equivalent Number) inayoanza na Herufi EQ kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).

Kwa maelezo ya ziada kuhusiana na sifa za waombaji na taratibu za utumaji wa maombi tafadhali kupitia: www.tamisemi.go.tz au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa namba za simu 026 2160210 au 0735 160210.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Mei, 2025 saa 05:59 usiku.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Comments (2)

Trackback URL | Comments RSS Feed

  1. Sisi wengine hatujasomea uwalimu naomba nafasi nyingine elimu yangu form four nida ninayo 0741421698
    0617885298 naombeni kazi

  2. Kelly Ramadan says:

    Naomba nafsi ya kujitolea kuwa mwalimu wa msingi nimeliza mwaka huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!