NAFASI Za Kazi Bumbuli District Council

Filed in Ajira by on May 30, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Kazi Bumbuli District Council

NAFASI Za Kazi Bumbuli District Council

NAFASI Za Kazi Bumbuli District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe
29/04/2025. Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 03

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada
(Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu
somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata programu za compyuta za ofisi kama vile:- Word,Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri.
  • Kupokea wageni na kuwasili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa.
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matuokio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
  • Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wajukumu ya kazi.
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika.
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinahusika.
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali – TGS C

✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 05

SIFA ZA MWOMBAJI
Awe na cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV), mwenye leseni daraja ‘C’ ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
  • Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
  • Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
  • Kufanya usafi wa Gari.
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.

NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali TGS B.

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI.

  • Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45 na umri usiopungua miaka 18.
  • Waombaji waambatanishe Cheti cha Kuzaliwa.
  • Waombaji waambatanishe amelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye Anuani, Namba za Simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees)
    wa kuaminika.
  • Waombaji wote waweke nakala za vyeti vya taaluma na vyeti vya Kidato cha Nne na Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali
    kwa kuzingatia sifa za kazi husika kwenye Ajira Portal.
  • Testimonials “Provision Results”, “Statement of Results” Hati ya Matokeo ya Kidato cha Nne na Sita HAVIKUBALIKI.
  • Waombaji wote waweke picha mbili “Passport Size” ya hivi karibuni katika ukurasa wa Ajira Portal.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vinahakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika yaani TCU, NECTA na NACTE.
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka wenye Kumb. Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 29 Novemba, 2010
  • Uwasilishwaji taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya Elimu, Anuani ya barua hiyo ielekeze kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli,
S.L.P. 111,
BUMBULI.

Maombi yote yatumwe kwenye Mfumo wa Kielekroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Secretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 09 Juni, 2025.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, GROUP NO 2 HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.


Tags:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *