NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma
NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma
Mganga Mfawidhi Wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni uwepo wa nafasi 5 za mkataba wa kujitolea kwa kada ya mtoa dawa za usingizi na ganzi (Anaesthest) kama ilivyo ainishwa hapo chini.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma ni hospitali inayotoa huduma za afya kwa wananchi wa mkoa wa Kigoma na maeneo mengine ya jirani.
Nafasi za kazi zinazotangazwa ni kama ifuatavyo:-
✅KADA: Mtoa dawa za Usingzi na ganzi (Anaesthests) NAFASI 5
MTOA DAWA ZA USINGIZI NA GANZI (ANAESTHESIA NURSE)
SIFA ZA MWOMBAJI
Waombaji wawe na stashahada ya uuguzi au wenye stashahada ya utabibu wenye mafunzo maalum ya anesthesia (utoaji wa dawa za usingizi) na vyeti vinavyotambulika katika taaluma husika.
KAZI NA MAJUKUMU YA MTOA DAWA ZA USINGIZI NA GANZI
- Kufanya kazi na vifaa vya kisasa vya anesthesia, kama mashine za kutoa dawa za usingizi na vifaa vya kufuatilia hali ya mgonjwa.
- Awe na Uelewa mzuri wa anatomia, fiziolojia, na farmakolojia, hasa kuhusu dawa za usingizi na athari zake kwa mwili wa binadamu.
- Kuchambua viashiria muhimu vya mgonjwa (mapigo ya moyo, shinikizo la damu, n.k.) na kuchukua hatua stahiki haraka ikiwa hali itabadilika.
- Kudhibiti mazingira ya dharura kama mgonjwa anapopata matatizo ya kiafya wakati wa usingizi wa dawa.
- Pamoja na kazi zingine za kitaaluma ambazo ataelekezwa na kiongozi/mwajiri wake
SIFA ZA JUMLA ZA MWOMBAJI
- Awe Raia wa Tanzania;
- Awe na Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45;
- Asiwe Mwajiriwa wa Serikali.
- kila mwombaji aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho wa taifa (NIDA).
- Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili na watakaoshindwa kuzingatia masharti ya tangazo hili hawataitwa.
- Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV), akionesha namba za simu na anuani yake na wadhamini 3 wa uhakika, vyeti vya elimu na taaluma.
- Mwombaji awe na uzoefu usio pungua mwaka mmoja (1) katika taaluma hiyo akiwa anafanya kazi, hivyo waombaji wenye uzoefu wa muda mrefu watapewa kipaumbele.
- Barua za maombi ziwasilishwe Pamoja na nyaraka zingine kama PDF File.
- Pia waombaji watakao tuma maombi yao nje ya muda na utaratibu maombi yao hayatafanyiwa kazi.
SIFA ZA KITAALUMA.
Waombaji wote wawe na vyeti vya elimu, vyeti vya taaluma, leseni kutoka baraza la taaluma husika.
MSHAHARA NA MARUPURUPU.
Waombaji watakaopata nafasi na kupewa mkataba watalipwa kwa kuzingatia Mwongozo wa kufanya kazi kwa kujitolea wa wizara ya Afya wa mwaka 2021.
MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA: –
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne au/na cha Sita kulingana na Kada ya Mwombaji.
- Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts) na Wasifu (C.V);
NB: Maombi yote yatumwe Kwa njia ya barua pepe (barua@mawenirrh.go.tz), au yapelekwe OFISI YA MGANGA MFAWIDHI kuanzia Tarehe 14/04/2025 hadi Tarehe 20/4/2025 Saa 09.30 alasiri.
Maombi yote yaelekezwe kwa;
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni,
S.L.P 16,
KIGOMA
MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA RUFAA YA MAWENI.
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma