NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma

Filed in Ajira by on March 11, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mganga Mfawidhi Wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma anawatangazia Watanzania wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni uwepo wa nafasi 1 ya mkataba wa kujitolea kwa kada ya fundi sanifu Bomba kama ilivyo ainishwa hapo chini.

✅FUNDI SANIFU DARAJA LA II – (TECHNICIAN GRADE II – PLUMBING) – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi za ufundi bomba atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

SIFA ZA WAOMBAJI

  • Waliohitimu wa kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya fundi bomba (Plumbing).
  • Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi bomba ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi Bomba.

SIFA ZA JUMLA ZA WAOMBAJI

  • Awe Raia wa Tanzania;
  • Awe na Umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45;
  • Asiwe Mwajiriwa wa Serikali.
  • kila mwombaji aambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho wa taifa (NIDA).
  • Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili na watakaoshindwa kuzingatia masharti ya tangazo hili hawataitwa.
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (CV), akionesha namba za simu na anuani yake na wadhamini 3 wa uhakika, vyeti vya elimu na taaluma.
  • Mwombaji awe na uzoefu usio pungua miaka mitatu (3) katika taaluma hiyo akiwa anafanya kazi, hivyo waombaji wenye uzoefu wa muda mrefu watapewa kipaumbele.
  • Barua za maombi ziwasilishwe Pamoja na nyaraka zingine kama PDF File. Pia waombaji watakao tuma maombi yao nje ya muda na utaratibu maombi yao hayatafanyiwa kazi.
  • Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
    Mshahara na Marupurupu.

Waombaji watakaopata nafasi na kupewa mkataba watalipwa kwa kuzingatia Mwongozo wa kufanya kazi kwa kujitolea wa wizara ya Afya wa mwaka 2021.

NB: Waombaji waambatanishe barua ya maombi na viambata vingine muhimu kwa Pamoja kama PDF na si vinginevyo.

Maombi yote yatumwe Kwa njia ya barua pepe (barua@mawenirrh.go.tz), au yapelekwe moja kwa moja OFISI YA MGANGA MFAWIDHI kuanzia Tarehe 10/3/2025 hadi Tarehe 17/3/2025 Saa 09.30 alasiri.

Maombi yote yaelekezwe kwa;
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni,
S.L.P 16,
KIGOMA

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!