NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe

Filed in Ajira by on January 24, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe

NAFASI Za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe, anapenda kuwatangazia nafasi za kazi, Watanzania wote wenye sifa zinazohitajika na wenye nia ya dhati ya kufanya kazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe nafasi husika ni kama ifuatavyo:-

✅AFISA HESABU MSAIDIZI DARAJA LA II NAFASI 2

Sifa za kuajiriwa: Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada katika fani ya Uhasibu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU:

  • Kuandika na kutunza “Register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
  • Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
  • Kutunza Majalada yenye kumbukumbu za hesabu.
  • Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu benki.
  • Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, hesabu za Benki na amana.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

MASHARTI YA UJUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

  • Muombaji awe Raia wa Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
  • Kila Muombaji anatakiwa ambatanishe wasifu “Curriculum Vitae yenye anwani sahihi, namba za simu sahihi, pamoja na majina mawili ya wadhamini (watumishi wa Serikali) na namba zao za simu zinazopatikana.
  • Barua za Wadhamini wawili zikiwa na anwani zao sahihi na namba za simu.
  • Awe na vyeti husika vya Taaluma, Testimonial “provisional results* “statement of results”, hati ya matokeo ya kidato cha nne HAVIKUBALIKI.
  • Waombaji waliosoma nje ya nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na TCU au NECTA.
  • Waombaji waambatanishe nakala za vyeti vifuatavyo vilivyothibitishwa:-
    1. Cheti cha kuzaliwa.
    2. Cheti cha kuhitimu elimu ya kidato cha nne.
    3. Cheti cha kuhitimu elimu ya kidato cha sita kwa waliohitimu.
    4. Cheti cha Taaluma.
    5. Picha ya Pasipoti 1.
    6. Leseni kutoka mabaraza husika.

Maombi yote yatumwe barua@songwerrh.go.tz
kwa njia ya email Baruapepe
Mganga Mfawidhi,
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe,
S. L. P 301,
SONGWE.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 31/01/2025.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!