Nafasi za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mt Walburga Nyangao

Filed in Ajira by on February 19, 2025 0 Comments
     
Nafasi za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mt Walburga Nyangao

Nafasi za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mt Walburga Nyangao

Nafasi za Kazi Hospitali ya Rufaa ya Mt Walburga Nyangao

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Hospitali ya Rufaa ya Mt. Walburga Nyangao iliyoko Jimbo Katoliki la Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Mtama inatangaza nafasi za kazi kama ifuatavyo;

✅Tabibu Meno II

SIFA ZA TABIBU MENO II
Wenye Stashahada ya Tabibu Meno kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi
  • Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida
  • Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo
  • Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya Msingi.
  • Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za Mfuko wa Afya ya Jamii.
  • Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma
  • Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi

✅Mteknolojia II – Mionzi (Radiografa)

SIFA ZA MTEKNOLOJIA II – MIONZI
Wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia katika fani ya radiolojia kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza pale inapohusika.

KAZI NA MAJUKUMU

  • Kuwapima wagonjwa wanaolekezwa kwenye eneo lake la kazi
  • Kutunza mitambo na vifaa vya Radiolojia katika eneo lake la kazi
  • Kukagua picha za X-Ray zilizopimwa kwa ubora na kutosheleza (diagnostic quality)
  • Kutunza picha za wagonjwa hadi majibu yanapowafikia madaktari waliowatuma wagonjwa
  • Kusimamia watumishi walio chini yake
  • Kutoa Ushauri kuhusu masuala ya na kazi za Radiolojia na Mionzi katika eneo lake la kazi.
  • Kuandaa vifaa vya tiba/uchunguzi na kusimamia utakasaji vifaa katika eneo lake la kazi (sterilization)
  • Kutoa mafunzo ya awali kwa watumishi wanaopangiwa kazi katika eneo lake la kazi.
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

✅Mtaalamu wa usingizi na ganzi (Anethetist)

SIFA MTAALAMU WA USINGIZI NA GANZI
Wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi au Utabibu na kupata kozi ya usingizi na ganzi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali,

SIFA ZA UJUMLA

  • Waombaji wawe ni raia wa Tanzania
  • Wawe na umri wa miaka 25-45
  • Waombaji waambatanishe cheti cha kuzaliwa
  • Waombaji waambatanishe maelezo binafsi (Detailed CV) na picha ndogo za karibuni (passport size)
  • Waombaji wenye uzoefu waonyeshe taarifa za taasisi walizofanyia kazi pamoja na waajiri wao

Maombi yote yaambatanishwe na vyeti vya taaluma na vyeti vya sekondari
Mshahara: Kadiri ya viwango vya serikali

Posho zingine: Makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa

Waombaji waandike maombi yao kupitia anwani ifuatayo;
MGANGA MFAWIDHI,
HOSPITALI YA RUFAA YA MT. WALBURGA NYANGAO,
S.L.P 1002,
NYANGAO, LINDI.

Maombi yanaweza wasilishwa kwa mkono kwa kuleta moja kwa moja au kupitia barua pepe nyangaohospital@gmail.com

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28/02/2024

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *