NAFASI Za Kazi Kishapu District Council

NAFASI Za Kazi Kishapu District Council
NAFASI Za Kazi Kishapu District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu anapenda kuwatangazia Wananchi wote wenye sifa kuomba ajira za Mkataba kwa nafasi ya Msaidizi wa Hesabu (Accounts Assistant), nafasi tatu (03).
Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kwa Wananchi wote wenye sifa.
SIFA ZA MUOMBAJI.
- Awe raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
- Awe amesoma masomo ya Uhasibu.
- Awe na cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA.
- Awe Mwaminifu.
- Awe na wadhamini wawili (2) waliothibitishwa kwa barua na kiongozi wa Serikali.
- Mwombaji awe na uzoefu wa kazi zaidi ya mwaka mmoja (1) katika fani hiyo.
- Awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
- Awe na afya njema na uwezo wa kufanya kazi vizuri.
KAZI/MAJUKUMU.
- Kuandika na kutunza “Register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
- Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
- Kutunza majalada ya Kumbukumbu ya Hesabu.
- Kupeleka nyaraka/barua za Uhasibu Benki.
- Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, hesabu za banki na amana.
Ngazi ya mshahara: Mwombaji atakayebahatika kuajiriwa kwa mkataba ataanza na mkataba wa malipo ya Tshs. 450,000/= kwa mwezi ngazi ya TGS B.
MASHARTI YA JUMLA.
- Awe tayari kufanya kazi kituo chochote cha Afya ndani ya Wilaya ya Kishapu.
- Mkataba utakuwa ni wa mwaka mmoja mmoja kwa kipindi chote na Mkataba utarudiwa kulingana na utendaji kazi na maadili ya mtumishi.
- Waombaji watakaokidhi vigezo wataitwa kwenye usaili.
- Mwombaji anatakiwa kuambatisha nakala ya vyeti halisi.
- Waombaji wote wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi/wasifu wake (CV), nakala za vyeti vyote vya elimu, nakala ya cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)/namba Passport size mbili (2) za hivi karibuni.
- Siku ya usaili kila mwombaji afike na vyeti halisi vya shule, taaluma, kuzaliwa na kitambulisho cha Taifa.
- Waombaji watakaowasilisha taarifa za kugushi watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.
- Kila mwombaji aandike kwa usahihi anwani yake na namba yake ya simu inayopatikana muda wote kwa ajili ya mawasiliano.
MUHIMU; Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na nakala ya viambata vyote muhimu.
Masharti yaliyoainishwa kwenye Tangazo hili yasomwe kwa umakini na yazingatiwe.
Maombi haya yawasilishwe kwa Anuani ifuatayo:-
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P. 1288,
22 Barabara ya DED-DC,
37582 KISHAPU.
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 15 Mei, 2025 Saa 9:30 Mchana
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
