NAFASI Za Kazi Madaba District Council

NAFASI Za Kazi Madaba District Council
NAFASI Za Kazi Madaba District Council
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba amepokea kibali cha Ajira chenye Kumb. Na. FA.97/288/01/A/25 cha tarehe 25/04/2025 kutoka kwa katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba anatangaza nafasi za kazi na anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi hizo kama ifuatavyo.
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 02
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa Kidato cha Nne (Form Four) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili. Aidha, wawe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja na kupata mafunzo ya programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powepoint, Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA MWANDISHI MWENDESHA OFISI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawadia na za siri.
- Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao na kuwaeleza wanapoweza kushughulikiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika
Idara/Kitengo/Sehemu husika. - Kukusanya, kutunza na kuyerejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya serikali TGS C1 kwa Mwezi.
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 07
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada au NTA level 6 katika fani ya utunzaji wa kumbukumbu, kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, na mwenye ujuzi wa Kompyuta.
KAZI NA MAJUKUMU YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming
correspondence register). - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence register).
- Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers).
- Kupokea majalada kwa Watendaji (action officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada(racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking).
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C1 kwa mwezi.
✅DEREVA DARAJA II – NAFASI 05
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving course) yanayotolewa na chuo cha VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
KAZI NA MAJUKUMU YA NAFASI ZA DEREVA
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi.
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara mishahara ya Serikali – TGS B1 kwa
mwezi.
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
- Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi yanafasi ya kazi kwa waajiri wao.
- Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Diploma/Certificates, – Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya Kitaaluma.
- “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili hayata shughulikiwa.
Barua ziandikwe kwa Anwani ifuatayo;-
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba,
38 Barabara ya Kifaguro Magingo,
S.L.P 10,
57186 MADABA, SONGEA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 09 Juni 2025.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
