NAFASI Za Kazi Mbarali District Council

Filed in Ajira by on April 16, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Kazi Mbarali District Council

NAFASI Za Kazi Mbarali District Council

NAFASI Za Kazi Mbarali District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali anawatangazia watu wote wenye sifa kuomba kazi ya nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
  • Awe mstaafu serikalini
  • Awe hajawahi kushitakiwa kwa kosa lolote la jinai
  • Awe na umri kuanzia miaka 55 hadi 65 (Sitini na Tano)
  • Awe na elimu ya Kidato cha Nne au cha Sita
  • Awe na taaluma ya kuanzia Stashahada ya juu/Shahada katika fani ya sayansi ya Jamii, Sheria, Utawala na Rasilimali Watu.

MAJUKUMU YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA

  • Kuendesha/Kuongoza vikao vya Usaili wa waombaji wa nafasi za kazi
  • Kuendesha/Kuongoza vikao vya kuwathibitisha kazini watumishi
  • Kuogoza/Kuendesha vikao vya kuwapandisha/kuwabadilisha watumishi vyeo.

POSHO
Kazi hii haina mshahara wa kila mwezi, Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira atakuwa analipwa posho kutokana na vikao vitakavyokaliwa na Bodi.

MASHARTI YA JUMLA

  • Mwombaji aambatishe wasifu wake kwenye barua yake ya maombi
  • Mwombaji aambatishe nakala halisi ya vyeti vyake vya elimu na taaluma
  • Kila mwombaji aambatishe maombi yake na picha 2 za passport size.

Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuanzia tarehe 16/04/2025 ya tangazo hili hadi tarehe 30/04/2025. Saa 9:30 alasiri.

Anuani ya kutuma ni:
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali,
S.L.P. 237,
RUJEWA-MBARALI.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *