NAFASI Za Kazi Mbeya District Council
NAFASI Za Kazi Mbeya District CouncilNAFASI Za Kazi Mbeya District Council
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anapenda kuwatangazia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kutuma maombi ya kuwa mjumbe wa Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri.
Bodi inatokana na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura Na 287. Bodi hiyo itakuwa Madarakani kwa kipindi cha Miaka mitatu (3).
Wajumbe wanaohitajika (wanaopigiwa kura)
- Wawakilishi wa watumiaji Huduma za Afya (Jamii) wanne kati yao wawili ni wanawake (nafasi 4)
- Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Afya za jamii (nafasi 1).
- Mwakilishi kutoka watoa Huduma za Afya binafsi (nafasi 1).
- Mwakilishi kutoka Taasisi/ Asasi za kijamii (Civil Society organization) watoa huduma za Afya (FBOs na NGOs) (nafasi 1).
Sifa za kuwa Mjumbe wa Bodi ya Huduma za Afya za Halmashauri.
- Awe ni Raia wa Tanzania.
- Awe na umri usiopungua miaka 21 na asizidi miaka 75. 3.
- Awe na Elimu ya kuanzia kidato cha Nne na kuendelea.
- Awe na akili timamu.
- Awe mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
- Awe Mwanachama hai wa Mfuko wa Jamii(CHF/TIKA).
MAJUKUMU NA KAZI ZA BODI ZITAKUWA KAMA IFUATAVYO:
- Itajadili na Kurekebisha Mipango ya Afya na Bajeti na kuiwasilisha kwa Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa.
- Itapokea, Kuchambua na Kuidhinisha taarifa za utekelezaji kutoka kwa Timu za Uendeshaji wa Huduma za Afya za Halmashauri.
- Itabuni Vyanzo mbalimbali vya mapato na kukusanya rasilimali za kutosha kuendesha huduma za Afya za halmashauri.
- Itasaidia Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri katika kusimamia rasilimali za Afya.
- Itashirikiana na Kamati za Afya za Vituo, Sekta binafsi na wadau wengine kwa nia ya kuinua kiwango cha Afya na utoaji wa huduma.
- Itaratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya Afya ikiwemo Mpango wa maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAMA) katika eneo la mamlaka husika; (eneo la halmashauri)
- Itaimarisha Miundombinu endelevu na Mfumo wa mawasiliano na usambambazji.
- Itahakikisha inakuwepo Wafanyakazi kulingana Halmashauri.
- Itawajibika kuandaa na kutekeleza mpango kazi wake.
- Itawajibika kufanya shughuli za ufuatiliaji na tathmini za utoaji huduma za Afya.
NAFASI Za Wajumbe wa Bodi ya Huduma za Afya Kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya
Barua za maombi zipitie Ofisi ya Mtendaji wa Kata kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya zikiwa zimeambatishwa na barua toka kwa Mtendaji wa Kijiji ikithibitisha kuwa wewe ni Mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
Kila Kata itachagua wajumbe wawili (2), mmoja wa Kiume na mmoja wa Kike kupitia Kikao cha WDC na kisha majina ya Wajumbe na barua zao za maombi yatawasilishwa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji kwa hatua Zaidi ndani ya siku saba (7) tangu tarehe ya mwisho ya kupokea maombi. (tarehe 1- 7 Aprili, 2025)
Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30.03.2025.
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

0756030841