NAFASI Za Kazi Mvomero District Council

NAFASI Za Kazi Mvomero District Council
NAFASI Za Kazi Mvomero District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero amepokea kibali cha Ajira mpya kwa ikama ya mwaka 2024/2025 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29/04/2025.
Hivyo Watanzania wote wenye sifa wanatangaziwa kutuma maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅DEREVA II – NAFASI 07
KAZI NA MAJUKUMU
- Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kuwapeleka Watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi,
- Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari.
- Kutunza na kuandika daftari la safari “log book” kwa safari zote.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kufanya usafi wa Gari.
- Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu kidato cha nne (IV) na kupata Cheti cha Mtihani wa Kidato cha Nne (IV). Awe na leseni daraja ‘C’ au “E” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila kusababisha ajali, Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya Uendeshaji Magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS – B
✅MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II – NAFASI 2
KAZI NA MAJUKUMU
- Kuorodhesha barua zinazoingia Masjala kwenye regista (incoming
correspondence register). - Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya taasisi (outgoing correspondence
register). - Kusambaza majalada kwa Watendaji (action officers).
- Kupokea majalada yanayorudi masjala toka kwa Watendaji.
- Kurudisha majalada kwenye shabaka/kabati la majalada (racks/filling cabinets) au mahali pengine yanapohifadhiwa.
- Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani ya Taasisi (file tracking)
SIFA ZA MWOMBAJI
Mwombaji awe na Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) aliyehitimu Stashahada (NTA level 6) katika fani ya Utunzaji wa kumbukumbu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, mwenye ujuzi wa Kompyuta.
NGAZI YA MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya mishahara ya Serikali – TGS C
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45.
- Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae) yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na
Anuani ya Barua Pepe (E-mail address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika. - Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo
mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. - Diploma/Certificates, – Cheti cha
mtihani wa Kidato cha IV na VI, – Computer Certificate, – Vyeti vya
Kitaaluma. - “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
MUHIMU. Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
na ielekezwe kwa anuani ya; –
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero,
S.L.P 663
MOROGORO
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hiipia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa
‘Recruitment Portal’).
Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 03 Juni 2025.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
