NAFASI Za Kazi Ruangwa District Council

NAFASI Za Kazi Ruangwa District Council
NAFASI Za Kazi Ruangwa District Council
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na.FA.97/228/01/A/25 cha tarehe 29.04.2025.
Watanzania wote wenye sifa zilizo ainishwa hapa chini, wanakaribishwa kuwasilisha maombi ya kazi kwa nafasi zifuatazo:-
✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI II – NAFASI 03
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amefaulu Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Aidha awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika moja na kupata Programu za Compyuta za Ofisi kama vile:- Word, Excel, Power point, Internet, E-mail na Publisher kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za Siri.
- Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaeleza wanapoweza kusaidiwa.
- Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine.
- Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya kazi.
- Kupokea majalada na kusambaza kwa maofisa walio katika Divisheni/Kitengo/Sehemu husika.
- Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika.
- Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya Ofisi.
- Kufanya majukumu mengine anayoweza kupangiwa na Mwajiri
NGAZI YA MSHAHARA: Watakao faulu usaili na kuajiriwa kwa nafasi hiyo watalipwa mshahara kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C
✅DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 11
SIFA ZA MWOMBAJI
Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Sita (Form Six), Awe na leseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Cource) yanayotolewa na Chuo cha VETA au NIT au Chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kukagua Gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari.
- Kupeleka watumishi kwenye safari za kazi.
- Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
- Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali.
- Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari.
- Kufanya usafi wa gari na
- Kufanya majukumu mengine ambayo atapangiwa na Mwajiri.
NGAZI YA MSHAHARA: Watakao faulu usaili na kuajiriwa kwa nafasi hiyo watalipwa mshahara kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B
MASHARTI YA JUMLA
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika pamoja na namba zao za Simu.
- Nakala hizo ziwe zimethibitishwa na Wakili au Kamishna wa Viapo.
- Testimonials, provision results, statement of results, havitakubaliwa.
- Waombaji wote ambao wamesoma Nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vinafanyiwa ulinganishi na TCU na NACTE.
- Waombaji waambatishe (Upload) picha moja Passport size ya hivi karibuni kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira.
- Mwombaji ambaye ni mtumishi wa Umma, lazima apitishe barua yake ya maombi kwa Mwajiri wake.
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
- Barua ya Maombi iandikwe kwa Kiswahili au Kiingereza
Barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa na mwombaji wa nafasi za kazi ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya,
15 Barabara ya Boma,
S.L.P 51,
65682 RUANGWA, LINDI.
MUHIMU: Maombi yote ya kazi yatumwe kwenye Mfumo wa Kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz/ na si vinginevyo. Anwani hii inapatikana pia kupitia kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kubofya ‘Recruitment Portal’.
Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFANYIWA KAZI.
Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 5 Juni 2025.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
