NAFASI Za Kazi Same District Council

Filed in Ajira by on May 2, 2025 0 Comments

     

NAFASI Za Kazi Same District Council

NAFASI Za Kazi Same District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

NAFASI Za Kazi Same District Council

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same amepokea Kibali cha Ajira Mpya kutoka kwa Katibu Mkuu – ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupitia baru ayenye Kumb. Na. FA.228/613/01F/072 ya tarehe 10.03.2025. Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa za kujaza nafasi tajwa hapo chini.

✅DEREVA DARAJA LA II (NAFASI 1)

MAJUKUMU YA KAZI

  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari;
  • Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;
  • Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari;
  • Kufanya usafi wa gari;
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au kujiandikisha.
  • Awe amehitimu Elimu ya kidato cha nne (IV) au sita (VI) awe na Lesseni ya Daraja la C au E ya uendeshaji wa magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
  • Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji wa magari ‘Basic Driving Course” yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA au NIT) au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
  • Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

NGAZI YA MSHAHARA TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI

  • Mwombaji awe raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45;
  • Mwombaji aambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika;
  • Mwombaji aambatishe cheti cha kuzaliwa kilichodhibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili;
  • Maombi yote yaambatane na cheti cha taaluma na nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho.
    – Certificates;
    – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI;
    – Vyeti vya kitaaluma (professional Certificates)
    – Picha moja ‘pasport size’ ya hivi karibuni;
  • Testimonials ‘provisional results’ results slip’ kiapo cha kuthibitisha umri wa kuzaliwa HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
    vii. Waombaji wa nafasi za ajira waliostaafishwa / kuacha kazi katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu
    Kiongozi;
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria;
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelezo yaliyo katika Waraka Na. CAC.45/257/01/D/140 wa tarehe 31 Novemba, 2010.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili hayatafikiriwa;

Mwombaji atatakiwa kuambatisha nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA) au namba ya NIDA kama hana kitambulisho;

Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa Ajira Aina ya ulemavu walionao;

Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu.

Anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Same,
S.L.P 38,
SAME

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielectroniki wa Ajira Recruitment Portal kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuto ya Seckretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa Kutuma Maombi ni tarehe 11 Mei, 2025.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!