NAFASI Za Kazi Singida District Council

Filed in Ajira by on April 17, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Kazi Singida District Council

NAFASI Za Kazi Singida District Council

NAFASI Za Kazi Singida District Council

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kuomba kazi ya nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira kwa kipindi cha mwaka 2025/2030.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe Raia wa Tanzania.
  • Awe mkazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
  • Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai.
  • Awe na umri kuanzia miaka 50 hadi 65 (sitini na tano).
  • Awe na Elimu ya Form IV au VI.
  • Awe na Taaluma ya kuanzia Stashahda ya juu/Shahada katika fani ya Sayansi ya Jamii, Sheria, Utawala na Rasilimaliwatu.

MAJUKUMU YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA

  • Kuendesha/Kuongoza vikao vya Usaili wa waombaji wa nafasi za kazi.
  • Kuendesha / Kuongoza vikao vya kuwathibitisha kazini watumishi.
  • Kuendesha / Kuongoza Vikao vya Kuwapandisha / Kuwabadilisha watumishi vyeo.

POSHO
Kazi hii haina mshahara wa kila mwezi, Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira atakuwa analipwa posho kutokana na vikao vinavyokaliwa na Bodi.

MASHARTI YA JUMLA

  • Mwombaji aambatanishe wasifu wake kwenye barua yake ya maombi.
  • Mwombaji aambatanishe nakala halisi ya vyeti vyake vya Elimu na taaluma.
  • Kila mwombaji aambatanishe maombi yake na picha 2 za passport size.

Maombi yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida kuanzia tarehe 14/04/2025 hadi tarehe 27/04/2025 saa 9.30 Alasiri.

Anuani ya Kutuma ni:
Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 27,
SINGIDA.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *