NAFASI Za Kujitolea Kukimbiza Mwenge Wa Uhuru 2025

NAFASI Za Kujitolea Kukimbiza Mwenge Wa Uhuru 2025
NAFASI Za Kujitolea Kukimbiza Mwenge Wa Uhuru 2025
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma inawatangazia Vijana wote wazalendo na walio tayari kuwania nafasi ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru, 2025 wenye Kauli Mbiu “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya. Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa na Sifa zifuatazo:-
SIFA ZA MUOMBAJI NGAZI YA MKOA (NAFASI MOJA)
- Awe na Umri kati ya miaka 18 hadi 35
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe Mzalendo na mwenye nidhamu
- Awe Mwenye afya njema
- Kipaumbele kitatolewa kwa muombaji ambaye hajawahi kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika ngazi ya Mkoa.
- Ikiwa amewahi kukimbiza Mwenge wa Uhuru kwenye ngazi ya Wilaya itakuwa sifa ya ziada.
SIFA ZA MUOMBAJI NGAZI YA WILAYA (NAFASI SITA)
- Awe na Umri kati ya miaka 18 hadi 35
- Awe Raia wa Tanzania
- Awe Mzalendo na mwenye nidhamu
- Awe Mwenye afya njema,
- Kipaumbele kitatolewa kwa muombaji ambaye hajawahi kukimbiza Mwenge wa Uhuru katika ngazi ya Wilaya
Maombi yanapokelewa katika Masjala Kuu iliyopo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma iliyopo Njedengwa kuanzia tarehe 24 February, 2025 hadi saa 28 February, 2025 saa 1:30 Asubuhi hadi saa 9:30 Alasiri.
Maombi yatumwe kwa kutumia Anuani ifuatayo:-
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,
Wilaya ya Dodoma,
1 Barabara ya Shekimweri,
S.L.P. 105,
41181 DODOMA.
Waombaji wote watakaokidhi vigezo na sifa, wataitwa kwenye Usaili utakaofanyika tarehe 11 Machi, 2025 na watalazimika kuja na vyeti halisi (Original Certificates) kulingana na sifa za Tangazo hili.
Aidha, barua za maombi ziambatishwe na Wasifu wa muombaji (Curriculum Vitae), Nakala za Vyeti vya Taaluma, Nakala ya Cheti cha kuzaliwa pamoja na Picha za Passport za rangi (2) zilizopigwa hivi karibuni, pia waombaji watatakiwa kuwasilisha Cheti cha utimamu wa Afya kutoka kwa Daktari/Mganga anaetambulika na Serikali.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
