NAFASI Za Mhandisi Mazingira Daraja la II MDAs & LGAs

Filed in Ajira by on March 27, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Mhandisi Mazingira Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI Za Mhandisi Mazingira Daraja la II MDAs & LGAs

NAFASI Za Mhandisi Mazingira Daraja la II MDAs & LGAs

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

✅MHANDISI MAZINGIRA DARAJA LA II (ENVIROMENTAL ENGINEER II) NAFASI – 1

MAJUKUMU YA MHANDISI MAZINGIRA DARAJA LA II

  • Kutoa ushauri wa namna ya kulinda mazingira kutokana na shughuli za Binadamu kama Kilimo, uvuvi, ufugaji nk
  • Kufanya Tathimini ya Mazingira (Environmental Impact Assesment) kwa miradi inayoanzishwa hasa ya Umwagiliaji na Uwekezaji katika Kilimo.
  • Kutoa ushauri wa namna ya kupunguza uharibifu wa Udongo utokanao na kemikali za madawa ya Kilimo, Pembejeo za Kilimo au Kemikali zingine za Viwandani zihusianazo na kilimo.
  • Kubuni vifaa na mikakati ya kuhakikisha kuwa maji taka na uchafu utokanao na kemikali zitokazo na Kilimo haziathiri Mazingira.
  • Kubuni mikakati itakayohakikisha kuwa Binadamu anaishi katika
    mazingira yenye Afya na Rafiki kimazingira.

SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya juu au Shahada ya Uhandisi Mazingira kutoka
Vyuo Vikuu au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na Serikali. Muombaji ni lazima awe amesajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).

NGAZI YA MSHAHARA -TGS E.

MASHARTI YA JUMLA.

  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na
    Mwanasheria/Wakili.
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya
    kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
  • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI Computer Certificate, Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa
pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
S. L. P. 2320, DODOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’).

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo
hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 07 Aprili 2025.

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *