Nafasi za Wahasibu na Makondakta Kaizirege and Kemebos Bus Service

Nafasi za Wahasibu na Makondakta Kaizirege and Kemebos Bus Service
Nafasi za Wahasibu na Makondakta Kaizirege and Kemebos Bus Service
Mkurugenzi wa kampuni ya mabasi ya abiria inayofanya safari zake kati ya Bukoba na Dar es Salaam kila siku anawatangazia nafasi za kazi kama ifuatavyo:
✅MAKONDAKTA WA MABASI
Sifa za Mwombaji
- Awe ni binti mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 25
- Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea
- Awe na uzoefu wa kufanya kazi kwenye mabasi ya abiria usiopungua mwaka mmoja
- Taaluma ya uhudumu wa abiria toka NIT ni sifa ya ziada
- Awe anajiamini na anaaminiwa na jamii iliyomzunguka
- Asiwe na historia yoyote ya kupatikana na kosa la jinai
- Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana, kujenga na kudumisha mahusiano mazuri na wadau wote wa kampuni
✅WAHASIBU
Sifa za Mwombaji
- Awe ni binti mwenye umri kati ya miaka 20 hadi 30
- Awe na stashahada au shahada ya usimamizi wa fedha na uhasibu kutoka katika chuo kinachotambuliwa na serikali
- Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili katika fani yake
- Ujuzi wa matumizi ya kompyuta ni sifa ya lazima
- Ujuzi mzuri wa uandishi wa taarifa za kifedha
- Utayari, ustahimilivu na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira atakayopangiwa na mwajiri.
Stahiki kwa nafasi hizi.
Ajira itakuwa ya mkataba na yenye mshahara na posho nzuri kwa watakaofuzu usaili.
Jinsi ya kushiriki usahili huu
- Usahili utafanyika siku ya Jumanne tarehe 18/02/2025 kuanzia saa 03:00 asubuhi kwenye ofisi zetu za kampuni zilizoko JIJINI DAR ES SALAAM, KINONDONI STUDIO kwa nafasi zote.
Waombaji wenye sifa na uhitaji wa nafasi hizi wafike siku ya usahili wakiwa na:
Barua ya maombi ya kazi ikielekezwa kwa:
Mkurugenzi,
Kaizirege and Kemebos Bus Service,
P.O. Box 1054, Bukoba au P.0. BOX 6633, KINONDONI, DAR ES SALAAM
- Wasifu binafsi (CV) wenye taarifa zote muhimu na sahihi za mwombaji pamoja na namba za simu zinazopatikana
- Wadhamini wawili waliotambulishwa na serikali ya mtaa kwa barua yenye picha ya kila mdhamini.
- Nakala ya vyeti vyote muhimu vya kitaaluma
- Picha mbili (Passport) za mwombaji za hivi karibuni
- Barua ya utambulisho wa mwombaji toka serikali ya mtaa unakotoka
Kwa maelekezo zaidi: 0677848343 au 0755760268 au 0714795465
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: Nafasi za Wahasibu na Makondakta Kaizirege and Kemebos Bus Service
Habar kwamaji yangu grecealisaliya natokeya kibamba naomba nafasi yau kondakta naomba sanaa Sina uzoefu wowo naomba mnisaidie Mimi grece kata yangu ni kibamba MTA kibwegelee wilaya ubungo naomba mnisaidie asnte sana🙏🙏🙏
Naomba nafasi ya kazi ya ukondakta kwenye kampuni yako kwani nitaifanya kwa uaminifu mkubwa.