NAFASI Za Walimu wa Fizikia na Hesabu Kagera

Filed in Ajira by on March 16, 2025 0 Comments
     
NAFASI Za Walimu wa Fizikia na Hesabu Kagera

NAFASI Za Walimu wa Fizikia na Hesabu Kagera

NAFASI Za Walimu wa Fizikia na Hesabu Kagera

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

NAFASI Za Walimu wa Fizikia na Hesabu Kagera, Nafasi za kujitolea kwa waalimu wa masomo ya Fizikia na Hesabu katika shule za sekondari za Mkoa wa Kagera.

Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) ni taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Usajili wa Wahandisi Sura ya 63.

Bodi hiyo ina majukumu ya kudhibiti tasnia ya uhandisi kwa kuwasajili na kuwaendeleza kitaaluma.

Aidha bodi inatambua umuhimu wa usawa wa kijinsia katika taaluma kwa kuhamasisha watoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hesabu (STEM) ili kuongeza idadi ya wahandisi wanawake.

Katika jitihada hizi, Bodi ilibaini changamoto ya walimu wa Sayansi katika shule za sekondari na inatekeleza mpango wa kufadhili ufundishaji wa Sayansi na Hisabati, STEM Support Program (SSP) kwa kufadhili walimu wa kujitolea kwaajili ya kufundisha masomo ya Fizikia, Kemia, Hesabu, na Biolojia.

Mradi huu unaratibiwa na ERB kwa ufadhili wa wadau wa maendeleo wakiongozwa na ubalozi wa kifalme wa Norway.

Hivi sasa, Bodi ya Usajili wa Wahandisi inatangaza nafasi za kujitolea kwa waalimu wa masomo ya Fizikia na Hesabu katika shule za sekondari za Mkoa wa Kagera, ambazo ni:

1. Shule ya Sekondari ya Kagera River
2. Shule ya Sekondari ya Kyerwa
3. Shule ya Sekondari Luteni Jenerali Silas Mayunga

VIGEZO VYA KUJIUNGA:

  • Mwalimu awe na shahada ya kwanza ya ualimu katika masomo ya Fizikia na Hesabu.
  • Awe tayari kufanya kazi katika Mkoa wa Kagera
  • Waombaji wanatakiwa kufaulu usaili ili kujiunga na mpango huu wa kujitolea.
  • Baada ya kuchaguliwa walimu wa kujitolea watalazimika kujiunga na TAeSA.

MUDA WA AJIRA:
Walimu hawa watakuwa na mikataba ya kujitolea kwa muda wa miezi sita, na mkataba utaongezwa kulingana na utendaji kazi.

Walimu Watalipwa posho ya kujikimu, Bima ya Afya, nauli ya kwenda kituo cha kazi, nauli ya likizo, na nauli ya kurudi kwao mara baada ya mkataba kumalizika.

JINSI YA KUUTUMA MAOMBI:
Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kwa njia ya barua pepe Kwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi, registrar@erb.go.tz wakieleza masomo wanayoweza kufundisha pamoja na nakala ya vyeti vyao vya kitaaluma na uzoefu.

Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi kupitia namba ya simu: 255 752060791 – Registrar, 255 757750130 – Eng. Veronica Ninalwo au barua pepe: registrar@erb.go.tz

Bodi ya Usajili wa Wahandisi inawakaribisha waalimu wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili kusaidia katika kukuza na kuendeleza elimu ya Sayansi na Teknolojia kwa watoto wa kike.

Tarehe ya kupokea maombi ni kuanzia 14 Machi 2025 hadi 31 Machi 2025.

TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!