Polisi Tabora Yathibitisha Kumkamata Ali kamwe

Polisi Tabora Yathibitisha Kumkamata Ali kamwe
Polisi Tabora Yathibitisha Kumkamata Ali kamwe
Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamshikilia Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe.
Hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao aliyesema kuwa jeshi hilo kumshikilia Ali Kamwe huku akitaja sababu kuwa ni kauli chafu kwa viongozi wa Serikali.
“Ndio tunamshikilia Ally Kamwe na tunaendelea na mahojiano na taratibu nyingine zitaendelea kwa mujibu wa sheria,”amesema Abwao.
Kamwe anashikiliwa ikiwa ni siku mbili zipite tangu arushe dongo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha katika hamasa kuelekea mchezo wao dhidi ya Tabora United uliomalizika jana Aprili 2, 2025 kwa Yanga kushinda bao 3-0.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha
Katika video inayosambaa mitandaoni inamuonyesha Kamwe akiwa mkoani Tabora akifanya hamasa ya mchezo huo huku akisema: “Kuna watu wanatafuta kiki..mkuu wa mkoa nani huyu, Chacha eenh? Atachacha kweli baada ya mechi,”
Chanzo cha Kamwe kusema hivyo ni kutokana na mkuu wa mkoa kuahidi Tabora United endapo itamfunga Yanga itapewa bonansi ya Sh60 milioni huku pia akishutumu watu wa Yanga kuwatumia meseji za rushwa wachezaji wa Tabora.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
