RAIS Karia Ajiuzulu CECAFA

RAIS Karia Ajiuzulu CECAFA
RAIS Karia Ajiuzulu CECAFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amejiuzulu rasmi nafasi ya Urais wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ili kuelekeza nguvu kwenye majukumu yake mapya ndani ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Karia ameacha kiti hicho muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.
Katika kipindi chake akiwa CECAFA, Karia alifanikiwa kuiinua kanda hiyo na kuifanya kuwa miongoni mwa bora ndani ya CAF, kwa maboresho makubwa ya mashindano na uongozi.
TFF imempongeza Karia kwa mafanikio hayo na mchango wake mkubwa katika kuleta heshima kwa taifa kupitia nyanja za kimataifa za soka.

Augustino Parek Maduot Rais Mpya wa CECAFA
Augustino Parek Maduot wa Sudan Kusini ndiye aliyeteuliwa Kukaimu nafasi hiyo Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Uamuzi huo umefanywa wakati wa Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika kwa njia ya mtandao May 2,2025 huku Maduot akitarajiwa kutumikia jukumu hilo hadi Mkutano Mkuu ujao wa Uchaguzi.
Maduot ambaye amekuwa akihudumu kama Makamu wa Rais wa CECAFA pia ndiye Rais wa sasa wa Chama cha Soka cha Sudan Kusini (SSFA).
Atakuwa na naibu wake Alexander Muyenge, Rais wa Shirikisho la Soka la Burundi.
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Matangazo ya kazi