RAIS Samia afanya Uteuzi Mpya 05 April 2025

RAIS Samia afanya Uteuzi Mpya 05 April 2025
RAIS Samia afanya Uteuzi Mpya 05 April 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Leo April 05, 2025 amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:-
Prof. John Wajanga Aron Kondoro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Prof. Kondoro anachukua nafasi ya Prof. Makenya Abraham Honoratus Maboko ambaye amemaliza muda wake;
Prof. Emanuel Amaniel Mjema ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kipindi cha pili.
Mhandisi Mwanasha Rajabu Tumbo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Mhandisi Tumbo anachukua nafasi ya Prof. Esnat Chaggu ambaye amemaliza muda wake.
IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Balozi Sirro anachukua nafasi ya Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo ambaye amemaliza muda wake.
Na Bi. Rosemary William Silaa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) kwa kipindi cha pili.
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
