RAIS Samia Apandisha Mshahara Kwa Watumishi 2025

Filed in Habari by on May 1, 2025 0 Comments
     
RAIS Samia Apandisha Mshahara Kwa Watumishi 2025

RAIS Samia Apandisha Mshahara Kwa Watumishi 2025

RAIS Samia Apandisha Mshahara Kwa Watumishi 2025, Sasa Kima Cha chini Cha Mshahara ni 500,000.

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1% mwaka 2025 ambapo kwa ongezeko hili sasa kima cha chini kitapanda kutoka 370,000 hadi 500,000.

Akiongea leo May 01,2025 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Mkoani Singida, Rais Samia amesema “Mwezi May mwaka jana wakati wa Siku ya Wafanyakazi Serikali ilieleza ugumu wa uchumi ulivyokuwa wakati ule na kuwasihi tusiongeze gharama kwa Serikali kwa kuongeza mishahara bali tuliendelea na upandishaji wa madaraja na kutoa maslahi mengine ya Wafanyakazi”

“Sasa kwa mapenzi makubwa na kwa namna mlivyoiunga mkono Serikali ilipowaomba mfunge mkanda na mkaamua kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kufanya uchumi wetu ukue kwa 5% mwaka huu, kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Wafanyakazi oyeee, miamvuli oyee, naona miamvuli imepanda sasa wakati wote ilikuwa chini sasa imepanda”

“Sasa kwakuwa Mcheza kwao hutunzwa, Mimi na wenzangu na baada ya kuangalia uchumi ulivyopanda na umepanda kwasababu ya nguvu zenu Wafanyakazi, ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba mwaka huu Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa Watumishi wa Umma kwa 35.1%, Wafanyakazi oyeee”

“Nyongeza hii itakayoanza kutumika mwezi July mwaka huu itaongeza kima cha chini cha mshahara kutoka 370,000 hadi Tsh. 500,000, ngazi nyingine za mshahara nazo zitapanda kwa kiwango kizuri jinsi bajeti inavyoruhusu lakini nataka niwaambie nyongeza nzuri ipo”

Kwa upande wa Sekta binafsi Rais Samia amesema kuwa bodi ya kima cha chini cha mshaharaa inaendelea kufanya mapitio ili kuboresha viwango vya chini vya mshahara kwa Wafanyakazi wa Sekta hiyo.

“Pamoja na kazi inayofanywa na Bodi hiyo, naendelea kuvihimiza Wizara na Vyama vya Wafanyakazi, kufanya majadiliano na Waajiri ili kutekeleza mikataba ya hali bora ya Wafanyakazi katika Sekta binafsi waendane sambamba na wenzao wa Sekta ya Umma”

“Ahadi yetu kwenu Wafanyakazi ni kwamba tutaendelea kuboresha mazingira ya kazi yakiwemo maslahi ya Wafanyakazi kadri hali ya uchumi itakavyoruhusu”

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *