Ratiba ya Mitihani ya Usajili na Taaluma kwa Wafamasia, Fundi dawa Sanifu, Fundi dawa Wasaidizi na Watoa dawa

Filed in Elimu by on February 15, 2025 0 Comments
     
Ratiba ya Mitihani ya Usajili na Taaluma kwa Wafamasia, Fundi dawa Sanifu, Fundi dawa Wasaidizi na Watoa dawa

Ratiba ya Mitihani ya Usajili na Taaluma kwa Wafamasia, Fundi dawa Sanifu, Fundi dawa Wasaidizi na Watoa dawa

Ratiba ya Mitihani ya Usajili na Taaluma kwa Wafamasia, Fundi dawa Sanifu, Fundi dawa Wasaidizi na Watoa dawa

MATANGAZO YA KAZI BOFYA HAPA

Baraza la Famasi linapenda kuwatangazia wahitimu wote wa kozi za famasi waliowasilisha maombi ya kufanya mitihani ya usajili na taaluma kuwa, mitihani hiyo imepangwa kufanyika tarehe 19-21 Februari, 2025 kuanzia Saa 02:00 asubuhi kwa utaratibu ufuatao:

Kila mtahiniwa atahitajika kuwa na NAKALA HALISI ya kitambulisho cha taifa au mpiga kura au leseni ya udereva au hati ya kusafiria kwa siku zote za mitihani.

Mtahiniwa atakaye shindwa kutimiza kigezo hiki hataruhusiwa kufanya mtihani.

Kila mtahiniwa anatakiwa kudurufu kadi yenye namba ya mtihani kutoka kwenye akaunti yake ambayo atatakiwa kuwa nayo wakati wote wa mitihani sambamba na vitambulisho vilivyoainishwa.

Kila mtahiniwa anatakiwa kuwa na kalamu ya bluu au nyeusi na nyekundu, kalamu ya risasi (pencil), rula na kikokotoo (calculator).

Aidha, watahiniwa wanakumbushwa kuhakikisha wanafika kwa wakati katika vituo walivyoomba.

Vituo vya kufanyia mitihani vitakuwa kama ifuatavyo:

  • Dar es Salaam – Kampala International University in Tanzania (KIUT)
  • Mwanza – Chuo Cha Afya na Sayansi Shrikishi MacWish-NYASHISHI.
  • Mbeya Chuo Kikuu Cha Teofili Kisanji (TEKU).
  • Dodoma – Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) – Shule kuu ya Tiba na Afya ya Kinywa (TIBA).
  • Arusha – Chuo Cha Uhasibu Arusha- NJIRO (Institute of Accountancy Arusha (IAA)

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi kupitia simu bila malipo namba 0736222503

Je, Unatafuta Nafasi za kazi?
Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA

JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *