RATIBA ya MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba

RATIBA ya MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba
RATIBA ya MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba
Baada ya kukwama kwa usafiri wa Meli tangu mwaka 2014 kati ya Mji wa Bukoba na Jiji la Mwanza Meli ya MV New Victoria hapa kazi tu ilianza safari zake tena kuanzia Agosti 16, 2020 kupitia Bandari ya Kemondo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Meli Tanzania (MSCL) alisema kuwa kutakuwa na nauli tofauti kulingana na madaraja yaliyopo, daraja la kawaida shilingi 21,000, Daraja la pili lenye vitanda vinne vya kulala shilingi 40,000, na watakao safiri daraja la kwanza watalipa shilingi 55,000.
“Muda wote wa safari abiria watapata huduma ya chakula na vinywaji katika migahawa na baa zilizopo katika madaraja yote” alisema Hamisi
Pamoja na Meli hiyo kuanza safari zake Meli nyingine iliyoanza safari zake ni MV Butiama.
Pamoja na Meli hizo kuanza kufanya kazi pia serikali inaunda Meli mpya ya Mv Mwanza miradi yote inagharimu kiasi cha sh 152 bilioni.
Ikumbukwe Meli ya MV Victoria ambayo sasa inaitwa MV New Victoria iliundwa mwaka 1965 na kusitisha huduma 2014 kutokana na uchakavu imegharimu zaidi ya sh 4.9 bilioni na inabeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo.
Hii hapa ni ratiba Kamili za MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba
- Mwanza to Bukoba Kupitia Badari ya Kemondo ni Jumanne, Alhamisi na Jumapili Saa 3:00 Usiku.
- Bukoba to Mwanza Kupitia Bandari ya Kemondo ni Jumatatu, Jumatano na Ijumaa Saa 3:00 Usiku.
Hizi hapa ni nauli za MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba.
- Daraja la Uchumi (Vijana/Watu Wazima) – 21,000.
Watoto – 11,000. - Daraja la Biashara (Vijana/Watu Wazima) – 40,000.
Watoto – 20,500. - Daraja la Kwanza (Vijana/Watu Wazima) – 55,000.
Watoto – 28,000.
Tazama zaidi hapa chini Ratiba na Nauli za MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba, Pamoja na NEW Butiama.

RATIBA na Nauli za MV Victoria Hapa Kazi tu Mwanza to Bukoba
TAZAMA AJIRA ZOTE TANZANIA
Je, Unatafuta Nafasi za kazi?Jiunge na Watanzania wengine Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku Kutoka Serikalini pamoja na Makampuni Mbalimbali.
Kupata Matangazo ya Ajira Kila Siku ni bure kabisa, JIUNGE HAPA
JIUNGE NA GROUP LETU HAPA, JIUNGE NA CHANNEL YETU HAPA, JIUNGE NA TELEGRAM HAPA.
